Ikiwa imewekewa lengo la kukusanya Sh12.054 kwa kipindi cha Julai 2015 hadi Mei 2016, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imefanikiwa kufikia malengo kwa kukusanya Sh1.032 trilioni kwa kipindi cha mwezi uliopita, ikiwa ni sawa na asilimia 100.7 ya lengo lililowekwa.
Akizungumza na
waandishi wa habari mjini Moshi, jana, Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata
alisema lengo lao kwa mwezi uliopita lilikuwa ni kukusanya Sh1.025 trilioni na
kwamba, kuanzia Julai 2015 hadi Mei 2016 wamekusanya Sh11.956 trilioni.
“TRA imejiwekea mikakati thabiti ya kuongeza
mapato kwa kipindi cha mwezi mmoja uliobaki ili kuweza kufikia au kuvuka lengo
kwa mwaka huu wa fedha na kwa sehemu kubwa tumeendelea kupambana na magendo,
hususan katika mipaka,” alisema Kidata.
No comments:
Post a Comment