Mbunge wa Shinyanga Mjini, Steven Masele
Hayo yameelezwa na Mbunge wa Shinyanga Mjini Steven Masele na
kutaka kauli ya serikali juu ya kukichukua kiwanda hicho kutoka kwa mwekezaji
na kuruhusu wananchi kulima eneo la kiwanda hadi hapo serikali itakapotatua
tatizo la kiwanda hicho kwani ahadi ya kukifufua ni ya miaka mingi.
Akijibu
swali hilo Waziri wa Viwanda Uchukuzi na Uwekezaji Charles Mwijage amesema
kwamba serikali inapitia viwanda 55 ambapo serikali imewataka waliobinafsishiwa
viwanda kuandika andiko la kibishara ili kuonyesha uwezo wao wa kuvifufua na
kuajiri na wakishindwa kufanya hivyo kwa muda waliopewa serikali itavitwaa
viwanda hivyo kikiwemo kiwanda cha nyama Shinyanga.
Aidha
kuhusu kuwapa wananchi wanaozunguka eneo la kiwanda kupewa eneo la kulima hadi
kitakapoanza kiwanda Waziri Mwijage amesema kwamba wananchi wasiguse maeneo
hayo ili mwekezaji asije kupata kigezo cha kutofufua kiwanda hicho alichowekeza
kisheria.
No comments:
Post a Comment