Tuesday, 7 June 2016

UKIMWI NI CHANZO KIKUBWA KINACHOPELEKEA VIFO KWA VIJANA WENGI

Pamoja na kuendelea kupungua kwa maambukizi ya ukimwi kutoka asilimia 5.7 mpaka 5.1 kwa mwaka 2011 na 2012,takwimu zinaonyesha kuwa bado kuna Vifo vitokanavyo na ukimwi na kwa bara la afrika Ukimwi ni chanzo cha kwanza kinachosababisha cha vifo kwa kundi la vijana.
Vijana wamekuwa na maambukizi makubwa hasa kuanzia miaka 15 -24 huku wasichana wakiwa katika hali ya hatari ambapo takwimu za mkoa wa Geita kutoka katika utafiti wa viashiria vya ukimwi na malaria za 2011/12 zinaonyesha kiwango cha maambukizi kwa wavulana ni asilimia 1.4 huku wasichana wakiwa na asilimia 4.3.

No comments:

Post a Comment