Mkuu wa mkoa wa
Geita,mh Ezekiel Kyunga,amewataka
wananchi na wazawa wa mkoani hapa kujenga destuli ya kuwekeza katika maendeleo
na kuacha destuli ya kuwekeza nje ya mkoa.
Wito huo ameutoa
katika uzinduzi wa hospatali ya Makoye wakati alipokuwa ni mgeni rasimi,amesema kuwa
kwa sasa Geita ni mkoa na sio wilaya kama ilivyokuwa hapo zamani hivyo ni vyema
kwa wazawa na wananchi wa maeneo mengine kuja na kuwekeza miradi ya
maendeleo mkoani hapa.
Aidha mkuu wa mkoa,ameongeza
kuwa kutokana na ugomvi ambao umeendelea kuwepo baina ya wafugaji na serikali
ni vyema kwa wafugaji kuona busara ya kuuza mifugo yao na kuwekeza katika
shughuli zingine ambazo zitaleta tija
kwa jamii.
Kwa upande
wake mkurugenzi wa hospitali hiyo,Makoye
Othuman,amewataka waandishi wa habari kuendelea kuutangaza mkoa wa Geita,na
kuwaelimisha wananchi juu ya athari za miamba taka maarufu kwa jina la
magwangala kuwa hayana faida kwa mkoa kwani wale ambao wanang’ang’ania ni watu ambao wanakuwa wanauhujumu mgodi.
Wananchi ambao
wamefika katika uzinduzi wa hospatali hiyo wamepongeza kwa juhudi ambazo
zimefanyika huku wakiamini kuwa huduma zitakazo tolewa zitakuwa ni za uhakika.
No comments:
Post a Comment