Tanzania huungana na nchi nyingine za kiafrika kuadhimisha siku ya mtoto
wa Afrika kila mwaka ifikapo june 16, lengo ikiwa ni kukumbuka mauaji ya watoto
waliouwawa kinyama na serikali ya makaburu na kusisitiza wajibu wa serikali za
Afrika kwa watoto ili kuendeleza haki na maslahi ya watoto nchini.
Mnamo mwaka 1990, uliokuwa umoja wa nchi huru za Afrika (OAU) ulipitisha
azimio la kuwakumbuka watoto wa kitongoji cha Soweto kilichopo Afrika ya kusini
waliouawa kinyama na iliyokuwa serikali ya makaburu ya nchi hiyo tarehe 16
juni, 1976 ambapo watoto hao walikuwa wakidai haki ya kutobaguliwa na haki
nyingine za kibinadamu.
Storm habari imezungumza
na wananchi mkoani Geita katika kuelekea siku ya maadhimisho hayo ambapo
wamesema kuwa sababu ambazo zimekuwa zikisababishwa kutokea kwa vitendo vya
ukatili kwa watoto ni pamoja na utumiaji wa madawa ya kulevya kwa baadhi ya
raia na kwamba serikali inapaswa kuhakikisha inachukua hatua kali kwa watu
wanaojihusisha na vitendo hivyo jambo ambalo litasaidia kutokomeza ukatili
nchini.
Maadhimisho haya huambatana na shughuli mbalimbali za maendeleo ambazo
hufanyika kitaifa na kimkoa na kwa mkoa wa Geita yatafanyika kesho katika
kijiji cha Lwamgasa kilichopo wilayani na mkoani hapa huku kauli mbiu ya mwaka
huu ikisema kuwa “ulawiti na ubakaji kwa watoto vinaepukika chukua hatua”.
No comments:
Post a Comment