Thursday, 18 February 2016

WANANCHI MKOANI GEITA WALALAMIKIA UWEPO WA SHIMO LA TAKATAKA LILILOPO KATIKATI YA MAKAZI YAO.

Uchafu ulivyofurika katika shimo hilo.
Wakazi wa mtaa wa katoma mkoani geita wamelalamikia uwepo wa shimo la taka lililopo katikati ya makazi yao huku wakiiomba serikali kuondoa kero hiyo ili kuepukana na magonjwa ya   mlipuko yanayoweza kutokea.

Storm habari imefika mtaani hapo na kujionea namna na jinsi wananchi hao wanavyokuwa wakipata suruba kutokana na uwepo wa shimo ilo ambalo limekuwa likitumika kutupia uchafu wa aina mbali mbali.

Wakizungumza na storm habari  baadhi ya wananchi wa eneo ilo, wameomba serikali kuiona hali hiyo na kuipatia ufumbuzi kwa kuliondoa shimo hilo kwani limekuwa  ni kero kwa muda mrefu kutokana na harufu mbaya ambayo imekuwa ikitoka katika shimo hilo hasa katika kipindi hiki cha mvua.

Storm habari imezungumza na mwenyekiti wa mtaa huo bw, Patrick Faida ambapo amekiri kuwepo wa kero hiyo mtaani hapo huku akidai kuwa suala hilo limekwishafika katika ofisi ya mkurugenzi mtendaji wa halimashauri ya mji  na muda wowote swala hilo litashughulikiwa.


Aidha  bw Faida, ameongea kuwa serikali inatambua umhimu wa utunzaji wa mazingira hivyo wanapashwa kuwa na subira huku akiwashauri kushirikiana kwa pamoja katika suala la usafi kwani jambo hilo ni jukumu la kila mwanachi.


Upande wa nje wa shimo hilo

No comments:

Post a Comment