Mkuu
wa kitengo cha Masoko na Uhusianao wa Wakala wa Uchimbaji Visima na Mabawa
(DDCA) Bw. Nungu Egwagwa akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani)
kuhusu
miradi iliyokwisha tekelezwa na wakala huo tangu kuanzishwa kwake ikiwemo
kuwezesha upatikanaji wa maji yenye ujazo wa mita zaidi ya milioni 23,000 kutokana na uchimbaji wa visima na Mabwawa.Kushoto ni Afisa Masoko na Uhusiano Bi. Ashura Katuga kutoka wakala huo.
miradi iliyokwisha tekelezwa na wakala huo tangu kuanzishwa kwake ikiwemo
kuwezesha upatikanaji wa maji yenye ujazo wa mita zaidi ya milioni 23,000 kutokana na uchimbaji wa visima na Mabwawa.Kushoto ni Afisa Masoko na Uhusiano Bi. Ashura Katuga kutoka wakala huo.
Wakala wa Uchimbaji
visima na Mabwawa (DDCA) Umewezesha
kupatikana kwa maji yenye ujazo wa mita zaidi ya milioni 23,000 kutokana na uchimbaji wa visima na mabwawa
uliofanywa na wakala huo katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Kauli hiyo imetolewa
leo Jijini Dar es salaam na Mkuu wa kitengo cha masoko na Uhusianao wa wakala
huo Bw. Nungu Egwagwa wakati akitoa taarifa kuhusu miradi iliyokwisha tekelezwa
na wakala huo tangu kuanzishwa kwake.
Akifafanua Egwagwa amesema kuwa lengo la wakala
huo ni kusaidia kutatua tatizo la upatikanaji wa maji kwa kuchimba visima na
mabwawa kwa gharama nafuu ambazo
wananchi walio wengi wanamudu.
“Tunachokifanya ni kutoa huduma
zaidi kuliko kufanya biashara kama Taasisi ya Serikali tukiwa na dhamira ya kusaidia
wananchi kuwa na visima na mabwawa yenye ubora unaotakiwa” Alisisitiza
Egwaga
Akizungumzia miradi
iliyotekelezwa na Wakala huo, Egwaga amesema kuwa mpaka sasa Wakala
umekwishajenga mabwawa 23 katika kipindi cha januari 1997 hadi june,2016 katika
mikoa mbamimbali ikiwemo Tanga,Shinyanga, Tabora, Mtwara naPwani.
Akitaja mikoa mingine
ambako mabwawa hayo yamejengwa Egwaga alisema kuwa ni Ruvuma,Manyara,Mbeya,
mwanza, Lindi na Mara.
Akitoa mfano wa miradi
ya uchimbaji visima Egwaga alisema kuwa moja ya miradi iliyotekelezwa ni ule wa
kuchimba visima katika chuo Kikuu cha Dodoma hali iliyosaidia kuondoa kabisa
tatizo la maji katika chuo hicho na katikamanispaa ya Dodoma.
Pia Egwaga alitoa wito
kwa watanzania kutumia huduma zinazotolewa na wakala huo ikiwemo kufanya
utafiti wa maeneo yanayofaa kuchimba visima virefu,kujenga malambo na
mabwawa,kupima wingi na ubora wa maji yatokayo kwenye visima na ujenzi wa
miradi midogomidogo ya mifumo ya usambazaji maji.
Madhumuni ya DDCA ni
kuongeza kasi ya kutafuta na kuviendeleza vyanzo vya maji kwa gharama nafuu ili
kuboresha huduma ya upatikanaji maji safai na salama na kutosha kwa matumizi
mbalimbali yakiwemo ya majumbani,mashambani,mifugo,ufugaji samaki na viwandani.
No comments:
Post a Comment