Polisi Wilayani Kahama
wametumia mabomu ya machozi kutawanya makundi ya wananchi wanaokutwa
wamekusanyika katika maeneo mbalimbali.
Mabomu hayo
yameendelea kurindima katika viwanja vya CDT ili kuwatawanya wananchi hao
waliokusanyika kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa hadhara wa Chadema.
Mkutano huo ulipangwa
kufanyika leo kuanzia saa 9.00 alasiri kabla ya polisi kuupiga marufuku na
jeshi hilo kuzuia mikutano mingine kama hiyo nchini.
Kupitia taarifa yake
kwa vyombo vya habari iliyotolewa jioni la leo na Kamishna wa Polisi Operesheni
na Mafunzo, Nsato Mssanzya amepiga marufuku maandamano na mikutano ya
hadharahadi hali ya usalama itakapotengemaa.
Amesema Jeshi la
Polisi halitasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa mtu yoyote au chama
chochote kitakachokaidi agizo hilo.
No comments:
Post a Comment