Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni akizungumza na mamia ya wananchi wa Kijiji cha Nyakabale, Kata ya
Mgusu, mkoani Geita ambao ni majirani wa Kampuni ya Uchimbaji wa Dhahabu ya GGM
mkoani humo. Wananchi hao wamelalamika kuwepo na vitendo vya ukatili dhidi yao
vinavyofanywa na baadhi wa askari wa kampuni hiyo. Hata hivyo Mhandisi Masauni
aliwataka Polisi mkoani humo kufanya uchunguzi wa haraka dhidi ya tuhuma hizo.
Mkazi wa Kijiji cha Nyakabale, Kata ya Mgusu, mkoani Geita,
Biosi Makongoro akitoa kero yake kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni (kushoto aliyekaa) dhidi ya Kampuni ya Uchimbaji wa
Dhahabu ya GGM mkoani humo ambayo ipo jirani na kijiji hicho, kuwa askari wa
kampuni hiyo wanadaiwa kuwanyanyasa wananchi hao wanapopita katika eneo la
Kampuni hiyo. Hata hivyo Mhandisi Masauni aliwataka Polisi mkoani humo kufanya
uchunguzi wa haraka dhidi ya tuhuma hizo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni (kulia) akiwasili Kituo cha Polisi Runzewe kilichopo Kata ya Uyovu
wilayani Bukombe ambacho Mbunge wa Jimbo hilo, Dotto Biteko aliuliza swali la
nyongeza Bungeni hivi karibuni akisema kituo hicho kinahitaji matengenezo makubwa
na kumuomba Naibu Waziri huyo kufanya ziara jimboni kwake kujionea kituo hicho.
Hata hivyo, Masauni alisema Serikali yake itahakikisha kituo hicho kitakuwa
katika hali nzuri.
Mkuu wa Kituo cha Polisi Runzewe kilichopo Kata ya Uyovu
wilayani Bukombe, Jackson Kirahuka akimuonyesha Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto aliyevaa koti) sehemu mbalimbali za
kituo hicho ambacho Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Dotto Biteko (katikati)
aliuliza swali la nyongeza Bungeni hivi karibuni akisema kituo hicho kinahitaji
matengenezo makubwa na kumuomba Naibu Waziri huyo kufanya ziara jimboni kwake
kujionea kituo hicho. Hata hivyo, Masauni alisema Serikali yake itahakikisha
kituo hicho kitakuwa katika hali nzuri. Aliyevaa Kaunda suti ni Mkuu wa Wilaya
hiyo, Amani Mwenegoha.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni (wa pili kushoto) akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja
Jenerali, Mstaafu Ezekiel Kyunga (meza kuu), Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini,
Joseph Msukuma (kulia), na Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani humo, Mponjoli
Mwabulambo, wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara ya kikazi mkoani humo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni akimfafanulia jambo Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Msukuma
(watatu kulia), na Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani humo, Mponjoli Mwabulambo
(wapili kushoto), wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara ya kikazi mkoani
humo.
Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akitoka ofisi ya Mkuu wa
Wilaya ya Bukendo, Amani Mwenegoha (kushoto) mara baada ya kumaliza kikao cha
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo iliyopo mkoani Geita. Naibu Waziri
alifanya ziara ya kikazi mkoani Geita.
No comments:
Post a Comment