Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo
Bw. Alex Nkenyenge akizungumza na wawakilishi kutoka Kampuni ya TING(hawapo
pichani) kuhusu kushirikiana na Serikali kuboresha mapato ya Uwanja wa taifa
kupitia matangazo.
Afisa Mtendaji Mkuu kutoka TING Mch.
Dkt. Veron Fernandos akifafnua jambo katika kikao kati ya kampuni yake na
Serikali kilicholenga kushirikiana katika kuboresha mapato ya Uwanja wa taifa
kupitia matangazo.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi
kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. william
Challe akichangia hoja katika kikao baina ya Serikali na kampuni ya TING
kushirikiana katika kuboresha mapato ya Uwanja wa taifa kupitia matangazo.
Mkuu
wa Masoko kutoka TING Bi. Bernice Hannah akionesha jinsi kampuni yake
itakavyoweka miundombinu ya kuweka matangazo ndani ya uwanja wa taifa katika
kikao baina ya Serikali na kampuni ya TING kushirikiana katika kuboresha mapato
ya Uwanja wa taifa kupitia matangazo.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Esther
Yonael kichangia hoja akichangia hoja katika kikao baina ya Serikali na kampuni
ya TING kushirikiana katika kuboresha mapato ya Uwanja wa taifa kupitia
matangazo.
Baadhi ya maafisa wa Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo wakifatilia kikao baina ya Serikali na kampuni ya
TING kushirikiana katika kuboresha mapato ya Uwanja wa taifa kupitia matangazo.
Serikali imeanza
majadiliano na kampuni ya TING katika kuboresha mapato ya uwanja wa Taifa
kupitia matangazo uwanjani hapo.
Akizungumza hapo jana
wakati wa kikao kati ya Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo na kampuni
hiyo, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Alex Nkenyenge
amesema kuwa Serikali imefarijika kupata maombi hayo kutoka kampuni ya TING ya
kuboresha mapato ya uwanja wa Taifa kupitia matangazo ambayo yatawekwa katika
maeneo ya uwanja huo.
“Ndugu zetu TING
wamekuja na wazo zuri sana na tumelipokea na tunaahidi kuliangalia kwa jicho la
tatu kwani ni fursa ya pekee kwetu, sio kuboresha mapato tu bali kutangaza
uwanja wetu na kuendeleza michezo kwa ujumla” alisema Bw. Nkenyenge.
Aliongeza kuwa ni
wakati sasa wa Serikali pamoja na Wananchi kufaidika na uwanja wao ambao ni wa
kipekee katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kwani fursa hiyo itasaidia
pia kuendeleza Kijiji cha Michezo Changamani ambao pia ni mpango wa Serikali
katika kuendeleza sekta ya michezo nchini.
Kwa upande wake Afisa
Mtendaji Mkuu kutoka TING Mch. Dkt. Veron Fernandos amesema kuwa kampuni yake
itatoa ushirikiano kwa Serikali kupitia Wizara na ni azma yao kuona wananchi
wanaona faida ya kuwa na uwanja wa kisasa ambao utawaletea mafanikio katika
maendeleo ya michezo nchini.
Kwa upande
wake Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani wa Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Esther Yonael ameipongeza kampuni ya TING kwa
kuona fursa na kuitumia kwani kuna kampuni nyingi zinaweza kuwa ziliona hiyo
fursa hii lakini sikakosa uthubutu wa kuleta maombi Wizarani kushirikiana
katika suala hilo ambalo linafaida kwa pande zote mbili.
Aidha, Mkuu wa Masoko
kutoka TING Bi. Bernice Hannah ameihakikishia Serikali kuwa wamejipanga vizuri
na wamefanya utafiti wa kina wa mradi huo na kuona kuwa unawezeka ukafanyika na
kuleta mabadiliko katika sekta ya michezo nchini.
Kampuni ya TING
imedhamiria kushirikiana na Serikali katika kuboresha mapato ya uwanja wa Taifa
na imejipanga kuwekeza Shilingi Billioni moja kwa miaka minne katika
miundombinu na wataalam.
No comments:
Post a Comment