Kutokana na kuwepo kwa vitendo vingi vya
ukatili kwa watoto kama kupigwa kulawitiwa na kubakwa, wazazi na walezi mkoani
Geita wametakiwa kushirikiana na viongozi mbali mbali ikiwemo polisi katika
kuhakikisha hali hiyo inatokomezwa.
Kauli hiyo imetolewa na afisa tawala wa
halmashauri ya wilaya ya Geita bi Janeth
Mobe alipokuwa akitoa hotuba kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya geita mh Manzie
Omary Manguchie ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya mtoto
afrika yaliyofanyika katika kijiji cha Lwamgasa kilichopo wilayani na mkoani
hapa.
Amesema kuwa jamii inatakiwa kushirikiana kwa
pamoja katika kutokomeza vitendo hivyo huku akilitaka jeshi la polisi kuongeza
doria na kwamba watuhumia wanaokamatwa kwa makosa hayo sheria ichukue mkondo
wake ili kokomesha hali hiyo.
Ameongeza kuwa halmashauri ya wilaya ya Geita
inazo kesi 66 zilizoripotiwa kuanzia
julai 2015 hadi june 2016 ambapo kesi za ubakaji ni 52 na ulawiti ni 2 na kwa
sasa kesi hizo ziko mahakamiani huku kesi 37 ziko katika upelelezi.
Kwa upande wao watoto waliohudhuria katika
maadhimisho hayo wameipongeza serikali kwa hatua ambazo imekuwa ikichukua huku
wakiiomba serikali kuendelea kukomesha hali hiyo kwa kuwafikisha mahakamani
wale wote wanaobainika kujihusihwa na vitendo viovu kwa watoto ili iwe fundisho
kwa watu wengine.
No comments:
Post a Comment