Mkuu wa mkoa wa Geita
meja jenerali mstafu Ezekiel Kyunga
amewataka wadau wa sekta ya usafiri wa umma kuakikisha wanafuata taratibu na sheria pindi wanapokuwa wakitoa
huduma kwa umma.
Akizungumza hivi
karibuni katika semina ya wadau wa sekta hiyo,Kyunga,amesema kuwa wakazi wengi
mkoani hapa wamekuwa wakitumia usafiri wa umma,lakini bado kumeonekana kuwepo
kwa changamoto na miongoni mwa
changamoto hizo ni wamiliki kushindwa kuelewa taratibu zilizolewa na mamlaka ya
usafiri nchini Sumatra.
Aidha kwa upande
wake,afisa sheria mkuu mamlaka ya udhibiti wa usafiri nchi kavu na majini
Sumatra,Leticia Mtaki,amesema kuwa kwa sekta ya upande wa bara bara wamekuwa na
changamoto nyingi na kubwa zaidi ni kutokana na miundo mbinu na baadhi ya watoa
huduma kutokuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani.
Mtaki,amewaomba watoa huduma kuhakikisha kuwa wanazingatia
sheria za usalama barabara lengo ikiwa ni kudhibiti ajali ambazo zimekuwa
zikijitokeza mara kwa mara.
No comments:
Post a Comment