Baadhi ya washiriki wa Warsha hiyo wakiwa katika kwenye ukumbi wa hotel ya Alphendo Mjini Geita wakati wa warsha ya kuwajengea uwezo wa watu wanaishi na VVU (WAVIU). |
Kulia ni Bw.Shilambele Mussa na Bi.Magdalena Ngwada wakifanya maigizo ya namna ambavyo mhudumu anaweza kutoa huduma kwa mtu mwenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi . |
MVIU mshauri Bi.Imelda Assey kutoka CTC ya hospitali ya wilaya ya Chato akisisitiza kuachana na dhana ya kuendelea kujinyanyapaa kwa watu wanaishi na VVU. |
Washiriki wakiwa kwenye vikundi wakijadili baadhi ya maswali. |
Mwezeshaji Bi.Amida Yindi akielekeza namna ambavyo MVIU mshauri anaweza kumhudumia mteja. |
Shirika lisilo la kiserikali
la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI)
linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) na UKIMWI kwa kushirikiana na Halmashauri za wilaya ya
Geita Vijijini,Geita Mji ,Chato na Bukombe limewakutanisha watu
wanaoishi na virusi vya Ukimwi (WAVIU Washauri)kwa lengo la kuwajengea
uwezo wa kutoa elimu na kuwaunganisha wateja kutoka kwenye jamii kwenda
kwenye vituo vya tiba na matunzo(CTC).
Warsha hiyo ambayo ilianza tarehe 29 January na inatarajia kumaliza
tarehe 31january 2018 inafanyika kwenye ukumbi wa hotel ya Alphendo mjini
Geita ikiwashirikisha washiriki 46 kutoka kwenye Halmashauri nne zilizopo
Mkoani humo.
Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa jamii kutoka Shirika la AGPAHI, Richard
Kambarangwe akizungumza wakati warsha hiyo amesisitiza kwa
WAVIU washauri kuunda vikundi kwenye CTC zao vya watu ambao
wanaishi na virusi vya Ukimwi ambavyo vitawasaidia kujiendeleza kwenye
shughuli za ujasiliamali pamoja na kushauriana katika matumizi ya dawa za
kufubaza makali ya VVU.
Kambarangwe ameeleza kuwa,kumeendelea kuwepo na tatizo kubwa la
unyanyapaa kwa watu wanaoishi na VVU hivyo kupitia warsha hii wamekuwa
wakifanya jitihada za kutoa elimu kwenye jamii kwa kupitia WAVIU washauri
ili kuondokana na dhana ya unyanyapaa.
Mmoja kati ya watu ambao wanaishi na VVU kwa muda wa miaka 15, Bw.
Eliya Malaki ambaye alipima VVU mwaka 2000 na kugundulika kuwa na
maambukizi alisema "bado kuna watu katika jamii hawaamini kuwa
wamepata maambukizi ya VVU matokeo yake wanakimbilia kwa waganga wa jadi na
wengine wamekuwa wakijinyanyapaa wenyewe kwa kushindwa kufika kwenye vituo vya
tiba na matuzo hili kupata ushauri na saa".
MVIU mshauri wa Bi. Imelda Assey kutoka CTC ya hospitali ya wilaya
ya Chato alisema "kupitia warsha
ambayo imefanywa na shirika la AGPAHI ni moja kati ya fursa ambayo itamsaidia
kuendelea kutoa elimu zaidi kwa watu ambao wanaishi na maambukizi ya Virusi vya
Ukimwi,huku akisisitiza jamii ya watu ambao wanaishi na maambukizi kuachana na
dhana ya kujinyanyapa bali kuikubali hali hiyo na kuzingatia ushauri ambao
wanapewa na wataalamu wa afya ".
Mwezeshaji katika warsha hiyo Bi,Amida Yindi ambaye ni mratibu wa
VVU na UKIMWI ngazi ya jamii kwenye halmashauri ya wilaya ya
Geita,amewasisitiza WAVIU washauri kujenga desturi ya kufanya usafi
kwenye vituo ambavyo wanafanyia kazi pamoja na kuangalia kadi za wateja kama
zimekusanywa na kuwekwa mahali ambapo ni sahihi.
No comments:
Post a Comment