Serikali imetangaza kuwatengea maeneo ya kuchimba wachimbaji
wadogo wa dhahabu waliopo karibu na mgodi wa dhahabu wa Geita Gold Mine (GGM)
uliopo mkoani hapa kwa ajili ya kuendelea na shughuli zao za uchimbaji ili
waweze kujipatia vipato.
Kauli hiyo imetolewa leo bungeni na naibu waziri wa nishati
na madini mh Medard Kalemani alipokuwa akijibu swali la mbunge wa viti maalumu
wa jimbo la Geita mjini bi Vick Kamata lililokuwa likiuliza kuwa ni lini
serikali itatenga maeneo kwa ajili ya wachimbaji wadogo wanaojishughulisha na
shughuli za uchimbaji mkoani Geita.
Kalemani ametaja maeneo hayo ni Mgusu, Nyakabale, Nyamalembo
ambapo maeneo ya Kasubuya serikali
imetenga hekta 432, Matabe hekta 568,
Chato hekta 1258 na 232 hekata Geita.
Akiendelea kutoa ufafanuzi juu ya swali la mbunge wa jimbo
la Geita mjini mh Cotantine Kanyasu lililoulizwa kwa niaba yake na mbunge wa
viti maalumu bi Vick Kamata lililouliza kuhusu wananchi kunyang’anya maeneo yao na kampuni ya Geita
Gold Mine (GGM) ambapo amesema kuwa kampuni hiyo ilifanya mazungumzo na
wananchi na kuweka makubaliano ya kuwalipa fidia wale wote walioko katika
maeneo ya kando kando na mgodi huo na kwamba baadhi yao wamekwisha lipwa fidia
zao.
No comments:
Post a Comment