Timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 (Serengeti
Boys) inataingia kambini Juni 13, 2016 kujiandaa na mchezo wa kufuzu fainali za
kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya vijana wenzao wa Shelisheli
utakaofanyika Juni 25, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Mchezo wa marudiano kati ya Serengeti Boys na Shelisheli
utachezwa Julai 2, 2016 huko Shelisheli.
Katika
kuajindaa na mchezo huo, Serengeti Boys ilifanya ziara India ambako walishiriki
mashindano ya vijana ya Kimataifa yanayotambuliwa na FIFA (AIFF International
Youth Tournament 2016) kabla ya kurudi na rekodi ya kupigiwa mfano si tu katika
Tanzania na kwa nchi za Afrika Mashariki.
Kadhalika
Serengeti Boys ilicheza mfululizo michezo saba ya kimataifa bila kufungwa dhidi
ya Misri (2), India, Korea Kusini, Malaysia na Marekani (USA). Kabla ya hapo
timu hiyo ilicheza michezo kadhaa ya ndani na timu za chini ya umri wa miaka 20
bila kupoteza hata mchezo mmoja.
Katika
mashindano ya AIFF, timu hiyo pekee kutoka Afrika na ambayo ilikua kipenzi cha
mashabiki katika jiji la Goha ilicheza na timu ambazo ziko juu katika hatua za
juu katika mtoano wa kuwania kushiriki Kombe la Dunia kupitia mabara yao yaani
CONCACAF (USA) na AFC (India, Korea na Malaysia)
Haishangazi
nchi nyingi za Ulaya, Asia na Marekani zimeulizia uwezekano wa timu hii
kutembelea nchi zao kwa michezo ya kirafiki.
Awali timu
ya Serengeti Boys ilipewa nafasi ndogo ya kufanya vizuri kwa sababu ya rekodi
zilizokuwa zinaiweka Tanzania katika viwango vya chini katika umri huo kwa nchi
za Afrika Magharibi na Kaskazini zilikuwa juu zaidi na vilevile ukweli wa
kwamba timu kama USA, Korea, Malasyia na India zilikuwa na bajeti kubwa
iliyogharamiwa na Serikali zao na walikuwa na vifaa vya kila namna kiasi cha
kuomba magari kwa ajili ya vifaa vya mazoezi na mechi.
Serengeti Boys ilimaliza Mashindano ya AIFF katika nafasi
ya tatu kwa kuifunga Malaysia mabao 3-0. Serengeti Boys na Bingwa Korea
hawakupoteza mchezo hata mmoja na awali walipokutana walitoka sare ya 2-2.
No comments:
Post a Comment