Naibu Waziri wa Habari,
Utamaduni, sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akisalimiana na Kaimu Meneja
wa Uwanja wa Taifa Bw. Julius Mgaya Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa
Taifa kupokea msaada wa mageti 27 kutoka kampuni ya TING yenye thamani ya Sh.
Million 44 kwa ajili ya kuweka vizuizi kulinda uharibifu wa miundombimu
uwanjani hapo.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, sanaa na Michezo Mhe. Anastazia
Wambura akisalimiana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Ting Dkt Vernon Fernandes mara
baada ya kuwasili katika uwanja wa Taifa kupokea msaada wa mageti 27 kutoka
kampui ya TING yenye thamani ya Sh. Million 44 kwa ajili ya kuweka vizuizi
kulinda uharibifu wa miundombimu uwanjani hapo.
Muonekano wa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam wenye uwezo wa kuingia
watu 60,000 waliokaa.
Serikali kupitia
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imepokea jumla ya mageti 27
kutoka Kampuni ya Ving’amuzi ya TING vyenye thamani ya Sh. Million 44.
Akizungumza wakati wa
kupokea msaada huo, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.
Anastazia Wambura ameushukuru Uongozi wa Kampuni ya TING kwa msaada mkubwa wa
mageti walioupata kwani utasaidia kutatua changamoto ya kukosa vizuizi vya
mageti katika Uwanja wa Taifa, ambapo kabla ilikuwa ikisababisha vifaa vingi
kuibiwa uwanjani hapo.
“Serikali na Wizara
yetu kwa ujumla inaishukuru sana kampuni yako kwa moyo wa utu na kujitolea kwa
manufaa ya Watanzania na wapenda michezo kwa ujumla” Alisema Mhe. Wambura.
Aliongeza kuwa, mara
baada ya kufungwa kwa vizuizi hivyo vya mageti katika uwanja huo, marekebisho
ya miundombinu iliyoharibiwa yatafanyika ili kurudisha hali ya usalama kwa
miundombinu hiyo.
Aidha, amewaomba wadau
wa michezo nchini kuiga mfano wa kampuni ya TING kwa kushirikiana na Serikali
katika kuboresha shughuli mbalimbali za michezo ili kuwezesha watanzania kupata
huduma bora na kuendeleza Michezo nchini.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Kampuni ya Ting, Dkt. Vernon Fernandes ameishukuru Serikali kupitia
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kukubali kushirikiana nao
katika kuboresha na kuendeleza sekta ya michezo nchini.
Msaada huo wa mageti
27 kutoka katika kampuni hiyo umekuja mara baada ya Naibu Waziri wa habari
Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura kutembelea uwanja wa Taifa
mapema mwaka huu na kujionea uharibifu wa miundombinu ambapo kampuni ya Ting
iliahidi kutoa mageti 26 kati ya 42 yanayohitajika.
No comments:
Post a Comment