Kesi iliyokuwa
inaunguruma kuanzia tarehe 29.02.2016 katika mahakam kuu jijini Arusha
imetolewa hukumu leo hii
Katika shauri hilo
aliyekuwa mgombea ubunge wa CCM jimbo la Longido Dr KIRUSWA alifikisha
mahakamni shauri hilo la kupinga matokeo ya ushindi dhidi ya mbunge wa Longido
mh ONESMO NANGOLE
Akisoma hukumu
hiyo,Jaji MWAGESI alisema kwamba mlalamikaji ndugu Kiruswa aliwakilishwa na
Wakili Dr.Masumbuko Lamwai na Wakili Haraka.
Katika shauri hilo,dai
la msingi la mlalamikaji bwana Kiruswa lilikua ni
1.Kutumika kwa lugha
ya matusi na kashfa wakati wa kampeni kutoka kwa mh Onesmo Nangole
2.Kuwepo kwa wapiga
kura kutoka nchi jirani ya Kenya walioletwa na Mh Nangole
3.kutumika kwa magari
ya Chadema kwenye kusindikiza na kubebea masanduku ya kupigia kura
4.Mkurugenzi wa
Uchaguzi kutangaza matokeo baada ya mgombea wa CCM kutolewa nje.
5.kutokea kwa vurugu
ndani ya chumba cha kuhesabu matokeo
Kutokana na madai hayo
na kwa kuzingatia kanuni,sheria na ushahidi uliotolewa pamoja na vielelezo na
mashahidi wa pande zote mbili,Jaji kutoka mahakama kuu Bukoba Mh.Jaji Mwagesi
alisema;
“Kutokana na
kuzingatia viini vyote vya shauri hili kama vilivyosikilizwa na kwa mujibu wa
sheria,Natamka kwamba;
Mahakama hii imetengua
shauri hili na kwa kujirisha kwamba mchakato mzima haukuwa wa haki."
No comments:
Post a Comment