Baada ya baadhi ya wabunge wa
upinzani kusimamishwa kuhudhuria vikao vya bunge kwa muda tofauti kwa madai ya
kukiuka kanuni za bunge.
Leo June 17 2016 idadi ya
wabunge kusimamishwa imeongezeka baada ya Naibu Spika, Tulia Ackson kutangaza
kusimamishwa kwa wabunge wawili ambao ni Mbunge wa viti Maalum CHADEMA
Suzan Lyimo na Anatropia Theonest.
Mbunge Suzan Lyimo
amesimamishwa na Bunge kuhudhuria vikao vitano vya Bunge baada ya kubainika
kusema uongo kwamba Jeshi la polisi nchini limenunua magari 777 ya washawasha
wakati ukweli ni kwamba hiyo ni Idadi ya magari inayopangwa kuingizwa na jeshi
hilo kwa ajili ya matumizi mbalimbali.
Licha ya Mbunge kuonesha
ushirikiano kwa kamati ya maadili, haki na madaraka ya bunge, kamati imemwona
Mbunge ni mzoefu wa shughuli za bunge hivyo anapaswa kusimamishwa vikao hivyo
kuanzia June 17 hadi 24 mwaka huu
Aidha Mbunge Anatropia Theonest
amesimamishwa kuhudhuria vikao vitatu vya bunge kwa kosa la kulidanganya Bunge
kuwa waziri wa ardhi na nyumba William Lukuvi alichukua ardhi ya wananchi akiwa
mkuu wa mkoa wa Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment