Nchini Kenya, virusi hatari aina ya FIV,
vinaavyofananana kabisa na virusi vya HIV vinavyosababisha Ukimwi vimegunduliwa
katika paka mmoja kupitia uchunguzi wa kimaabara.
Hii ni baada ya uchunguzi wa kina wa damu ya paka huyo
kuthibitisha uwepo wa viini vinavyofanana kabisa na vile vinavyoathiri
binaadamu.
Wafugaji wa paka na wanyama wa nyumbani wameonywa
kuwapeleka wanyama wao kufanyiwa uchunguzi wa afya wanapowashuku wanyama wao
wanaugua.
Virusi hivyo vinaitwa FIV (Feline Immunodefficiency
Virus).
Ugonjwa huo sio mgeni katika wanyama.
Mwaka wa 1986 madaktari nchini Marekani
waligundua virusi vilivyofanana kwa karibu na vile vinavyoambukiza binadamu vya
HIV.
Lakini hii ndio mara ya kwanza kwa virusi hivyo
kugunduliwa nchini Kenya.
Madaktari wa maabara ya Lancet mjini Nairobi Waligundua
kuwa virusi hivyo vinasababisha ukosefu wa kinga mwilini na kudhoofisha afya ya
wanyama hao wanaopendwa na kuishi majumbani.
Hata hivyo waliwahakikishia wafugaji wa paka kuwa hakuna
ushuhuda wowowte wa maambukizi kutoka kwa paka hao kwenda kwa binadamu.
Daktari Dhaval Shah badala yake amewashauri wafugaji wa
paka kuwafungia paka wao ndani ilikuwazuia wasijamiane na wale paka
wanaorandaranda mitaani ambao huenda wameambukizwa ukimwi wa paka.
“kimsingi ugonjwa huu ni Ukimwi wa waka, japo
inaambukizwa kupitia kwa mate na mkwaruzano haswa paka wanapopigana''
No comments:
Post a Comment