Baadhi ya wananchi Mkoani Geita bado hawaona kuwa uzaaji
watoto wengi kuna athari kwa maendeleo ya nchi na kiafya kwa ujumla huku baadhi
yao wakidai kuwa wamehalalishwa kuzaa hadi kizazi kitakapoisha.
Matumizi ya uzazi wa mapango hasa vijijini bado ni changamoto
huku baadhi ya kaya zenye watoto wengi wanashindwa kuwapa mahitaji kama ya
chakula,mavazi pamoja na huduma zingine kutokana na kuwa na watoto wengi huku
wazalishaji katika familia ni wachache.
Baadhi ya wakazi mkoani hapa wanaona kuzaa ni tunu bila
kujali athari za kiafya na kiuchumi na matatizo ya uzazi wa mpango mkoani geita
hadi sasa ni asilimia 26 tu, na changamoto zimekuwa zikiwakumba baadhi ya
wanawake wanapotaka kutumia njia hizo za uzazi wa mpango huku maeneo ya mjini
kidogo kuna uelewa kwa jamii tofauti na kijijini
Utafiti uliofanyika hivi karibuni unaonyesha kuwa
utumiaji sahihi wa njia za uzazi wa
mpango unasaidia kupunguza vifo kwa wajawazito kwa asilimia 40, msikilize
mganga mkuu wa wilaya ya chato Alhamis Nyamagubi akielezea kuhusu hili
Takwimu za mkoa zinaonyesha waliopata ushauri wa huduma
ya uzazi wa mpango ni wanawake kumi na nane elfu na arobain na tano, huku
waliopata njia ya uzazi wa mpango baada ya kujifungua ni moja elfu mia sita
thelathini na tano na waliopata uzazi wa mpango baada ya mimba kuharibika ni
165 na mwsho waliopata rufaa ya kwenda kliniki ya uzazi wa mpango ni moja elfu
na mia tattu sitini na moja hata hivyo elimu bado inahitajika zaidi kwa jamii
kuhusu Matumizi ya njia za uzazi wa mpango ili kuboresha hali ya familia na
uchumi wa Taifa kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment