Mkurugenzi Msaidizi Maji Shirikishi kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji
Bw. Sylivester Matemu akiongea na waandishi (hayupo pichani) kuhusu Maadhimisho
ya 6 ya Wiki ya Maji Barani Afrika na Mkutano wa 10 wa Baraza la Mawaziri wa
Maji wa Nchi za Afrika utakaofanyika kuanzia tarehe 18-22 Julai 2016. Kulia ni
Afisa Mawasiliano wa Wizara hiyo Bw. Dennis Kiilu.
Tanzania Mwenyeji maadhimisho ya 6 ya wiki ya Maji Barani Afrika
na Mkutano wa 10 wa Baraza la Mawaziri wa Maji wa Nchi za Afrika
yatakayofanyika Julai,2016 Jijini Dar es salaam
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Msaidizi Maji
Shirikishi kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji Bw. Sylivester Matemu wakati wa
mkutano na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam.
Mgeni Rasmi katika Ufunguzi wa Maonyesho ya Wiki ya maji
yatakayofanyika kabla ya mkutano wa Baraza la Mawaziri atakuwa Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa.
Akifafanua Matemu amesema kuwa mkutano huo utahusisha washiriki
zaidi ya 1000 kutoka mataifa 54 kutoka Bara la Afrika na wengine
kutoka nje ya Afrika.
Maadhimisho hayo yataambatana na maonyesho ya
shughuli za wadau wa sekta ya maji na umwagiliaji, kwenye Ukumbi wa Kimataifa
wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es salaam.
Kauli mbiu ya kongomanao hilo ni “ Kufikia lengo la maendeleo
Endelevu Juu ya usalama wa Maji na usafi wa mazingira” alibainisha Matemu.
Mkutano huo utawasaidia wataalamu wa maji kutoka
Mataifa mbalimbali ya Afrika kujadiliana kuhusu mikakati mbalimbali
itakayosaidia kupambana na changamoto zinazoikabili sekta ya maji katika bara
la Afrika.
Akizungumzia faida za Mkutano huo Matemu amesema kuwa utasaidia
kufungua fursa mbalimbali zilizopo katika sekta ya maji na Sekta nyingine
ikiwemo kukuza na Kutangaza vivutio vilivyopo hapa nchini hali itakayosaidia
kukuza Utalii.
No comments:
Post a Comment