Mkuu wa idara ya kilimo na mifugo
halmashauri ya wilaya (DALDO) Chato na mawakala wa pembejeo za kilimo
wamehukumiwa kwa makosa ya rushwa .
Mahakama ya wilaya ya Chato mkoani
Geita imewatia hatiani na kuwahukumu washitakiwa 4 kwa makosa mbalimbali ya
uhujumu uchumi, katika kesi 4 tofauti.
Waliotiwa hatiani na
kuhukumiwa kati ya washitakiwa wengine
walioachiwa huru ni aliyekuwa mkuu wa idara ya kilimo na mifugo (DALDO) wilayani
Chato dk. Fares Nyamsimbwa Tongora pamoja na waliokuwa mawakala wa pembejeo za
kilimo wa wilaya hiyoo bw. Sephania Endelyasi Mahenge na bi Mary David Mwamgogwa.
Washitakiwa
walipatikana na hatia na kuhukumiwa tarehe 6/6/2016 mbele ya hakimu mfawidhi wa
mahakama ya wilaya ya Chato mh.Jovith Kato na mwendesha mashitaka wa takukuru bw Kelvin Murusuri
katika mashauri tofauti ya uhujumu uchumi ma 4 kati ya ma 5 yaliyotolewa uamuzi
ambayo ni ecc 01/2015, ecc 01/2014, ecc 04/2013, na ecc 06/2013.
Washitakiwa walikuwa
wanakabiliwa na makosa ya rushwa yaliyotokana na ugawaji wa pembejeo za kilimo
kwa wananchi katika msimu wa kilimo wa mwaka 2010/2011.
Dk. Fares Nyamsimbwa Tongora
alipatikana na hatia na kuhukumiwa jumla ya makosa 12 ya kula njama ili kutenda
kosa, kusaidia kutenda kosa, na matumizi mabaya ya madaraka ya umma kinyume na
vifungu namba 30, 31, na 32 sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya
mwaka 2007.mshitakiwa atahukumiwa kwenda jela
miaka 12 au kulipa faini jumla ya tsh. million 2 ,000,000/= . mshitakiwa
alilipa faini .
Mh.Jovith Kato alieleza
kwamba dk. Fares Nyamsimbwa Tongora alishindwa kutimiza majukumu yake kwa
uzembe hivyo kusababisha serikali kushindwa kuwafikishia wakulima pembejeo za
kilimo na serikali kuwalipa mawakala fedha ambazo hawaku kustahili.
Aidha wakala wa
pembejeo bw.Sephania Mahenge alitiwa hatiani na mahakama kwa jumla ya makosa 40
katika kesi 2 ambazo ni namba ecc 01/2015 na namba ecc 06/2013 na kuachiwa huru
katika kesi namba ecc 05/2013.
Naye bi Mary David Mwamgogwa alikutwa na hatia
katika makosa 40 katika kesi za uhujumu uchumi namba ecc 04/2013 na ecc 1/2014,
ambapo mawakala wote wawili bw. Sephania Mahenge na bi Mary Mwamgogwa walitiwa
hatiani kwa makosa ya kughushi nyaraka
kinyume na vifungu na 333,335 na 337 na kutengeneza nyaraka za uongo kinyume na
kifungu cha 342 vyote vya sheria ya
kanuni ya adhabu( cap 16 ya mwaka 2002).
Mahakama ilimhukumu
bw.Sephania Mahenge kulipa faini jumla
ya tsh.laki 900,000/= au kwenda jela jumla ya miaka 4 kwa makosa 40 ya kesi 2
alizopatikana na hatia. mshitakiwa alilipa faini.
Hata hivyo mahakama
haikuweza kusoma adhabu dhidi ya bi Mary David Mwamgogwa kwa sababu ya
kutokuwepo mahakamani na itasoma atakapopatikana.
Mkuu wa takukuru mkoa
wa Geita bw. Thobias Ndaro ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa geita kuendelea
kuiunga mkono takukuru na serikali kwa ujumla katika mapambano dhidi ya rushwa
kwa kutoa taarifa mbalimbali za vitendo vya rushwa na ubadhilifu katika miradi
mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na vitendo vinavyofanyika kwenye ofisi
za serikali za mitaa, mahakama na halmashauri ili watuhumiwa waweze kuchukuliwa
hatua za kisheria na hivyo kushiriki kutokomeza vitendo vya rushwa, ubadhilifu
na ufisadi katika jamii zetu na hivyo mwananchi atakuwa ameshiriki kukata
mnyororo wa rushwa.
No comments:
Post a Comment