Mabingwa mara mbili
mfululizo wa kombe la Mataifa ya Ulaya timu ya taifa ya Hispania imefanikiwa
kufuzu hatua ya 16 bora baada ya kuichapa Uturuki kwa bao 3-0 kwenye mji wa
Nice, Ufaransa.
Wakionesha kiwango cha
juu kwenye michuano, Spain wamekuwa timu ya kwanza kufunga magoli zaidi ya
mawili kwenye mechi za michuano ya Euro 2016.
Alvaro Morata
aliifungia bao Spain kwa kichwa kisha Nolito akaongeza bao lingine kwa shuti
kali la karibu.
Goli la tatu
lilipatikana baada ya kupigwa pasi 21 likijumuisha wachezaji tisa kisha Morata
akaweka mpira kwenye neti.
Spain kwenye ubora wao
Spain waliingia kwenye
mchezo wakiwa na kumbukumbu ya kushinda mchezo wao wa ufunguzi wa michuano ya
Ulaya kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2008 wakati Uturuki wakiwa wanakosolewa
kwa kiwango chao duni kwenye mchezo waliopoteza dhiudi ya Croatia na mchezo wao
dhidi ya Spain ukamalizika kama wengi walivyotarajia.
Kikosi cha Hispania
hakijapoteza mchezo dhidi ya Uturuki kwa miaka 62 sasa huku wakiwa hawajafungwa
katika mechi 13 zilizopita kwenye fainali za kombe la Ulaya, walitawala mchezo
na walikuwa hawazuiliki.
Gerard Pique na
Nolito, walikaribia kufunga kabla ya mshambuliaji wa Juventus Alvaro Morata
kuunganisha kwa kichwa krosi ya Nolito na kuipatia bao Spain.
Turan azomewa na
mashabiki wake
Kikosi cha Fatih Terim
kimekuwa kikikosolewa pamoja na star wake Arda Turan baada ya kichapo cha bao
1-0 kwenye mchezo wao wa ufunguzi na huenda mambo yakawa mabaya zaidi baada ya
kipigo kingine kutoka kwa Spain.
Kipindi cha pili
mashabiki wa Uturuki walimzomea kiungo wao na klabu ya Barcelona baada ya star
huyo kupooza shambulizi la counter-attack lakini nyota huyo alijibu mapigo kwa
kuwaonesha dole gumba.
Mashindano haya ni
machungu kwa Turan ambaye alinunuliwa na Barcelona kwa ada ya euro milioni 40
akitokea Atletico Madrid lakini alijikuta akizomewa na mashabiki wa taifa lake
tangu mchezo dhidi ya Croatia.
Dondooo muhimu
Kadi ya njano aliyooneshwa Sergio Ramos
sekunde ya 58, imekuwa kadi ya mapema zaidi kwenye michuano ya Euro tangu
Aleksandrs Isakovs kwenye mchezo wa Latvia dhidi ya Germany sekunde ya 40,
ilikuwa mwaka 2004.
Nolito amekuwa mchezaji wa sita tofauti wa
Spain kwenye historia ya michuano ya Euro kufunga na ku-assist kwenye mchezo
mmoja akiungana na Pereda, Cesc Fabregas, Dani Guiza, David Silva pamoja na
Fernando Torres.
Uturuki hawajapata clean sheet kwenye michuano
ya Euro tangu waliposhinda 2-0 dhidi ya Belgium kwenye michuano hiyo mwaka
2000, wamefungwa magoli 15 kwenye mechi nane tangu wakati huo.
Morata anakuwa mchezaji wa tano kufunga
kuanzia magoli mawili kwenye michuano ya Euro akiwa kwenye timu ya taifa na
kuungana na Alfonso Perez, David Villa (hat-trick v Russia), Fernando Torres
and Xabi Alonso.
Spain hawajapoteza mechi kwenye michezo yao 14
ya michuano ya Euro (W11 D3), huku wakiwa hawajaruhusu goli ndani ya dakika 690
No comments:
Post a Comment