Ikiwa leo
ni siku
ya kukumbuka watu wenye uaribino
duniani,wananchi mkoani Geita wameiomba serikali kuhakikisha
inaweka mipango madhubuti katika
kutokomeza mauaji yanayohusisha watu wenye ualibinism nhini
Storm habari imezungumza na baadhi ya wananchi ambapo
wamesema kuwa kumekuwepo na tabia ya baadhi ya watu kuwaua kwa madai ya kupata mali jambo ambalo halina
ukweli wowote na kwamba serikali
inatakiwa kuweka mikakati madhubuti ili kuthibiti suala hilo kwa kutoa
elimu kwa wananchi itakayosaidia
kukomesha vitendo hivyo.
Hata hivyo storm habari imezungumza na kamanda wa
jeshi la polisi mkoani Geita Mponjoli Mwabulambo,ambapo amesema kuwa jeshi la
polisi limekuwa likitumia mbinu mbalimbali ili kuthibiti mauaji hayo kwa
kuwatumia polisi jamii ambao wapo kuanzia ngazi ya vitongoji, ikiwemo pia
viongozi wa dini.
Aidha kamanda ametoa wito kwa wananchi kuachana na
imani potofu zinazosababishwa watu kufanya vitendo hivyo huku akiwataka
kushirikiana na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa pindi wanapokuwa na mashaka
na baadhi ya watu wanaodaiwa kujihusishwa na vitendo hivyo.
Siku ya albinism duniani ni siku ambayo
inaadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe 13 june lengo ikiwa ni kutoa elimu kwa
watu wenye albinism na kutoa uelewa zaidi kwa watu hawa.
No comments:
Post a Comment