Saturday, 4 June 2016

BOXER MAHIRI WA ZAMANI ULIMWENGUNI MUHAMMAD ALI AFARIKI DUNIA

Boxer mahiri wa zamani wa uzito wa juu ulimwenguni Muhammad Ali amefariki dunia huko katika hospitali ya Phoenix iliyopo jimbo la Arizona nchini Marekani.
Muhammad Ali (74) maarufu kwa jina la ‘The Greatest’, alikuwa amelazwa katika hospitali ya Phoenix tangu Alhamisi ambao muongeaji wake Bob Gunnell alisema kwamba Ali alikuwa akisumbuliwa na tatizo la mfumo wa upumuaji.
Bingwa huyo wa zamani wa uzito wa juu mara tatu pia alikuwa akisumbuliwa na tatizo la kiharusi tangu mwaka 1984.
Katika miaka ya hivi karibuni, Ali alikuwa haonekana mara kwa mara hadharani. Mara ya mwisho alionekana April 9 huko Phoenix kwenye hafla fupi ya uchangishaji fedha kwa ajili ya waathrika wa kiharusi. Hii ni kwa mujibu wa Jamhuri ya Arizona (Arizona Republic), na katika hafla hiyo Ali alionekana kuvaa miwani nyeusi.
Enzi za ujana wake hakufahamika tu kama mpiganaji hodari aliyeshinda ubingwa wa uzito wa juu mara tatu, lakini pia kwa uanaharakati wake mbele ya jamii.
Historia yake kwa ufupi
Ali alizaliwa huko Louisville katika jimbo la Kentucky nchini Marekani January mwaka 19942 akijulikana kwa jina la Cassius Clay. Alianza kujihusisha na masuala ya masumbwi alipokuwa na miaka 12 tu na ndipo mwaka 1964 akatwaa ubingwa wa kwanza wa uzito wa juu kwa kumtwanga kwa ‘knockout’ Sonny Liston. Mwaka huo huo aliamua kubadili dini na kuwa Muislam.
Maisha yake ya masumbwi yaliingiwa na 3½ ya dosari mnamo mwaka 1960, wakati alipokataa kujiunga na jeshi la Marekani wakati wa vita dhidi ya Vietnam, hali iliyopelekea kushtakiwa, lakini hata hivyo mahakama kuu iliitupilia mbali kesi hiyo.
Baada ya hapo alishinda ubingwa wa uzito wa juu mara mbili kabla ya kustaafu mwaka 1981.


No comments:

Post a Comment