Thursday, 23 June 2016

BAADHI YA WANANCHI WA KIJIJI CHA BUKUNGU MKOANI GEITA WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KUCHUKUA SHERIA MKONONI



Kamishna msaidizi wa Jeshi la polisi mkoani Geita Mponjoli Mwabulambo.



Moja ya nyumba zilizobomolewa na wananchi.

Katika hali isiyo ya kawaida wananchi wenye hasira kali wa kijiji cha Bukungu Kata ya Buzirayombo mkoani Geita wamevamia na kubomoa nyumba kwa madai kuwa watu hao wamekuwa wakifanya uhalifu wa kuvamia wanakijiji katika nyumba zao na kuwaibia mali na fedha hali iliyopelekea kuwahisi kuwa wao ndo wahalifu.


Kamishna msaidizi wa Jeshi la polisi mkoani Geita Mponjoli Mwabulambo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mpaka sasa watu kadhaa wanashikiliwa na Jeshi la polisi wanaosadikika kuhusika na ubomozi wa nyumba hizo.

Pia alitoa wito kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi na hivyo kuacha vyombo vya usalama vifanye kazi yao.

No comments:

Post a Comment