Jeshi la polisi mkoani Geita limezuia matembezi ya amani ya yaliyoratibiwa na chama cha ACT wazalendo yaliyokuwa
yamepangwa na viongozi wa chama hicho ngazi ya mkoa, lengo ikiwa ni kuunga mkono
harakati zinazofanywa na kiongozi wa chama hicho Taifa, Mh.Zitto Kabwe.
Jeshi hilo limepiga
marufuku huku likiwaandikia barua viongozi wa chama hicho, sababu kubwa
zilizotajwa kuzuia matembezi hayo ni
kupisha maandalizi ya mwenge wa uhuru na sababu nyingine ikitajwa kwamba
kutakuwa na mwingiliano wa oparesheni zinazoendelea mkoani hapa.
Storm habari
imezungumza na Katibu wa Chama hicho
mkoani hapa Bwana Ikolongo Emmanuel Otoo,ambapo amesema kuwa wanasikitishwa na
taarifa ambayo imetumwa na jeshi hilo huku wakiendelea kukiona chama tawala
kikiendelea na mikutano mkoani hapa..
Hata hivyo Storm
habari imeshuhudia gari la kikosi cha
kutuliza ghasia cha FFU siku ya jana likirandaranda mtaani kwa masaa kadhaa
kuimalisha hali ya ulinzi dhidi ya uwepo wa tarifa hizo ambapo matembezi hayo
yalikuwa yamepangwa kuanza majira ya saa tatu asubuhi mpaka saa kumi na moja jioni
yakianzia katika uwanja wa Nyankumbu hadi uwanja wa magereza mjini humo.
Aidha wananchi Mkoani
hapa wamekuwa na maoni na mitazamo tofauti juu ya kile ambacho kiliweza
kuendelea.
Storm habari imemtafuta
Kamishina msaidizi wa polisi mkoa wa geita mponjoli mwabulambo na amesema kuwa maandamano yoyote yale yanahitaji
askari na sababu ambazo wamezitoa ni za msingi na ni vyema zikazingatiwa katika
suala zima la ulinzi na usalama.
No comments:
Post a Comment