Wabunge wote wa vyama vya upinzani leo tena wametoka nje kupinga Naibu
Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson kuendesha vikao vya Bunge na kumwachia
Bunge yeye na wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Taarifa kutoka Bungeni
zinaeleza kuwa, wabunge wote wa upinzani wametoka nje kususia kikao cha Bunge
ikiwa ni kutekeleza azimio lao la kutokuwa na imani na Dk Tulia.
Baada tu ya kusomwa
dua ya kufungua Bunge, wabunge hao wametoka nje majira ya saa 3:00 asubuhi
na kumwacha Dk. Tulia akiwa na wabunge wa CCM pekee.
Kambi
upinzani ilianza utaratibu huo juzi kwa kutoka ndani ya ukumbi wa Bunge
baada ya Dk. Ackson kuingia ukumbini.
Kiongozi wa Kambi
Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, juzi alisema wataendelea kutoshiriki
vikao vinavyoongozwa na Naibu Spika hadi pale "haki itakapopatikana."
No comments:
Post a Comment