Ikiwa ni siku
chache tangu kuadhimisha siku ya mtoto wa Afrika imebainika vitendo vya
ukatili dhidi ya watoto bado ni tatizo katika jamii nzetu ambapo katika mtaa wa
Msalala road kata ya Kalangalala ,mkoani
hapa mama anayejulikana kwa jina la Janeth Yohana, amekuwa akiwafungia ndani
watoto wenye umri wa mwaka mmoja na miezi saba
ambao ni mapacha na yeye kwenda katika vilabu vya pombe za kienyeji.
Storm habari ilifanikiwa kufika katika mtaa huo na
kuona mazingira ambayo wanaishi watoto hao kuwa si mazingira ya kuridhisha
kwani ndani kulikuwa ni kuchafu na watoto wakiwa katika hali ya upweke na
simazi.hata hivyo baadhi ya majirani wamesema kuwa ni desturi na tabia ya mama
huyo kuwaacha watoto hao na kwamba walisha wahi kumshauri mama huyo lakini amekuwa
ni mgumu wa kuelewa.
Aidha kwa upande wake diwani wa kata ya Kalangalala,Sospeter
Mahushi,amesema kuwa kuhusu tuhuma za kufungiwa ndani watoto hao hakuwa nazo mpaka
pale alipotafutwa na mwandishi wetu na kwamba maamuzi ambayo atayafanya
atamwagiza mtendaji aweze kuwakamata wazazi wa watoto hao huku wakishughulikia
njia ambavyo wanaweza kuwatafutia namna ya kuwatunza watoto hao.
Hata hivyo katika hali isiyo ya kawaida mama huyo huwa
anapokea pesa za ruzuku ambazo ni za TASAF,na
amekiri kupokea fedha hizo na kwamba pindi anapopokea huwa ananunulia mahitaji
ya nyumbani na mpaka sasa ni awamu nne amekwisha kupokea.
Hadi Storm habari inaondoka eneo la tukio iliacha
watoto hao wamechukuliwa na msamalia ambae alikuwa ni jirani wa mama huyo huku
mama huyo akipelekwa katika dawati la jinsia lililipo kituo cha polisi.
No comments:
Post a Comment