Mke
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akisalimiana na
baadhi ya viongozi wa Chama cha watu wenye Ulemavu wa Ngozi Mkoa wa Lindi walipomtembelea
leo asubuhi kwa ajili ya kupokea msaada wa mafuta ya kujikinga na mionzi ya jua
kwa watu wenye ulemavu wa ngozi.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli na Mke wa
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa wakifurahia
jambo na mtoto mwenye ulemavu wa ngozi walipomtembelea leo asubuhi Ikulu ndogo
Mkoani Lindi kwa ajili ya kupokea msaada wa mafuta ya kujikinga na mionzi ya
jua kwa watu wenye ulemavu wa ngozi..
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akiongea na
jamii ya watu wenye ulemavu wa ngozi walipomtembelea leo asubuhi Ikulu ndogo
Mkoani Lindi kwa ajili ya kupokea msaada wa mafuta ya kuzia mionzi ya jua kwa
watu wenye ulemavu wa ngozi ambapo aliiasa jamii kujali kundi hili na kuacha
imani potofu dhidi yao. Kulia ni Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mama Mary Majaliwa na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh. Godfrey
Zambi
Mke wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akimkabidhi Mwenyekiti
wa Chama cha watu wenye Ulemavu wa Ngozi Mkoa wa Lindi Bw. Hemed Said mafuta ya
kuzuia mionzi ya jua kwa watu wenye ulemavu wa ngozi leo Ikulu ndogo ya Mkoa wa
Lindi.Katikati ni Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama
Mary Majaliwa
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli
akikabidhi zawadi ya mbuzi na kuku kwa Mwenyekiti wa Chama cha watu wenye
Ulemavu wa Ngozi Mkoa wa Lindi Bw. Hemed Said walipomtembelea leo asubuhi Ikulu
ndogo Mkoani Lindi kwa ajili ya kupokea msaada wa mafuta ya ngozi kwa watu
wenye ulemavu wa ngozi.Kulia ni Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mama Mary Majaliwa
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli, Mke wa
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa na Mkuu wa
Mkoa wa Lindi Mh. Godfrey Zambi wakiwa katika picha ya Pamoja na jamii ya watu
wenye ulemavu leo asubuhi Ikulu ndogo Mkoani Lindi.
No comments:
Post a Comment