Meja
Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga( katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe James Ihunyo
Watumishi wa Serikali Wilayani
Bukombe mkoani Geita wametakiwa kufanya kazi kwa bidii na waledi ili kuleta
maendeleo katika halmshauri hiyo.
Hayo yamesemwa na Afisa
tawala Mkoani hapa, Selestine
Gasimba katika Baraza maalumu la kujibu hoja za CAG amesema kuwa nyakati
zimebadilika hivyo ni vyema kujua kuwa wakati wa kufanya mambo kimzaa wakati
huo umekwisha ni vyema kwa watendaji wakaongeza faida ya kufanya kazi kwa bidii
zaidi.
Mkuu wa wilaya hiyo, Amani Mwenegoha amesema kuwa Halmashauri
ambayo inatakiwa kujibu hoja za CAG ni halmashauri ambayo haijasimamia vizuri
watendaji wake.
Diwani wa kata ya Uyovu, Yusuf Fungameza na Diwani wa Viti maalum
Elizabeth Ngasa wamewalalamikia
wataalamu kufanya kazi kwa mazoea na kusababisha halmashauri yao kupoteza
mali na mapato sanjari na hilo la kupewa na CAG hati ya mashaka.
No comments:
Post a Comment