Serikali imewasilisha Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2016/2017 ya Sh trilioni 29.53, ambayo
nguvu kubwa imewekwa katika kukusanya mapato kwa kulinda viwanda vya ndani na
kubana matumizi ya serikali ili kuelekeza sehemu kubwa ya matumizi katika
maeneo ya vipaumbele.
Katika
bajeti hiyo, bidhaa za lazima zinazogusa maisha ya wananchi ikiwemo mafuta ya
petroli na dizeli pamoja na ushuru wa barabara na maji ya kunywa, havijaguswa
huku bidhaa za starehe kama bia, sigara, soda, juisi na nyingine kama nguo za
mitumba, huduma za kupanga nyumba na uhamishaji fedha kwa simu, vikipandishwa
kodi, huku kiinua mgongo cha wabunge, kufutiwa msamaha wa kodi.
Aidha,
makusanyo ya mapato yasiyo ya kodi, ikiwemo mapato ya taasisi za udhibiti kama
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Mafuta (EWURA), Shirika la Viwango
(TBS), Jeshi la Polisi (Trafiki) na mamlaka nyingine za udhibiti, sasa
yatapelekwa moja kwa moja katika Mfuko Mkuu wa Serikali ambapo mahitaji yao ya
fedha yatatolewa na Wizara ya Fedha na Mipango, badala ya kujigawia kutokana na
bakaa ya mapato waliyokusanya.
Aidha,
maduka ya kutoa huduma katika majeshi, yamefutiwa kodi rasmi na badala yake,
Serikali inajipanga kuongeza posho kwa askari, ili iwasaidie kukidhi mahitaji
yao, huku taasisi za umma na ofisi zote za Serikali, zikipigwa marufuku kufanya
biashara na mzabuni asiyetumia mashine za kodi za kielektroniki (EFD’s).
Kodi
juu,
Katika
bidhaa zilizoongezewa ushuru na kodi ni pamoja na vinywaji baridi, kutoka Sh 55
kwa lita mpaka Sh 58, huku ushuru wa forodha katika maji ya matunda (juisi)
yanayotumia matunda yanayozalishwa hapa nchini, ukipanda kidogo kutoka Sh 10
mpaka 11 kwa lita. Juisi zinazotokana na matunda ambayo hayazalishwi hapa
nchini, ushuru wake pia umepanda kutoka Sh 200 kwa lita hadi Sh 210 kwa lita.
Kwa
upande wa bia, serikali imependekeza bia inayotokana na nafaka ya hapa nchini,
ambayo haijaoteshwa kama kibuku, ushuru upande kutoka Sh 409 kwa lita mpaka
430.
Bia
zingine, ushuru wake pia umepanda ambao sasa utatoka Sh 694 mpaka 729 kwa lita,
huku bia zisizo na kilevi, ikiwa ni pamoja na vinywaji vya kuongeza nguvu,
ushuru ukipanda kutoka Sh 508 kwa lita mpaka Sh 534.
Kwa
upande wa mvinyo uliotengenezwa kwa zabibu zilizolimwa nchini kwa kiwango cha
asilimia 75, ushuru wake umepanda kutoka Sh 192 kwa lita mpaka Sh 202.
Ushuru
wa mvinyo unaotengenezwa na zabibu zilizolimwa nje ya nchi kwa kiwango
kinachozidi asilimia 25 kutoka Sh 2,130 kwa lita mpaka Sh 2,237. Vinywaji vikali
havikuachwa nyuma maana ushuru umepanda kutoka Sh 3,157 mpaka Sh 3,315.
Sigara
zisizo na kichungi zinazotengenezwa kwa tumbaku ya hapa nchini kwa kiwango
angalau asilimia 75 kutoka Sh 11,289 hadi Sh 11, 854 kwa kila sigara
1,000.
Kwa
upande wa sigara zenye kichungi zinazotengenezwa kwa tumbaku ya nchini kwa
angalau asilimia 75, ushuru juu kutoka Sh 26,689 hadi Sh 28, 024 kwa kila
sigara 1,000.
Sigara
zenye sifa tofauti na hizo, ambazo hazina vigezo hivyo vya tumbaku ya ndani,
ushuru wake umepanda kutoka Sh 48,285 hadi Sh 50,700 kwa kila sigara 1,000.
Katika
tumbaku ambayo iko tayari kutengenezwa kuwa sigara, ushuru wake umeongezeka
kutoka Sh 24,388 hadi Sh 25,608 kwa kilo huku ushuru wa sigara aina ya Sigar
ukibaki kuwa asilimia 30.
Katika
mafuta ya kulainisha mitambo, ushuru umepanda kutoka Sh 665.50 kwa lita hadi Sh
699 kwa lita, huku ushuru wa grisi za kulainisha mitambo, ukipanda kutoka senti
75 kwa kilo, hadi senti 79 kwa kilo.
Gesi
asilia pia ushuru umepanda kutoka senti 43 kwa futi za ujazo mpaka senti 45 kwa
futi za ujazo.
Kuhusu
viwango vya ushuru wa kuhamisha fedha kwa kutumia simu, serikali imependekeza
kutoza ushuru wa asilimia 10, kwenye ada zinazotozwa na watoa huduma wa simu,
katika kutuma na kupokea fedha, badala ya ushuru huo kutozwa tu katika kutoa
fedha.
Kwa
mujibu wa Dk Mpango, kwa utaratibu wa sasa, baadhi ya kampuni zinazotoa huduma
zimetumia mwanya wa kuhamisha sehemu kubwa ya ada hizo kwenye kupokea fedha na
hivyo kuwa nje ya wigo wa kodi.
Kwa
upande wa kiinua mgongo cha wabunge wakati wa kustaafu, sasa kitatozwa kodi
kila mwisho wa muhula wa miaka mitano ili kujenga misingi ya usawa na haki
katika utozaji wa kodi kwa kila mtu anayestahili kulipa.
Aidha,
mapato yote yatokanayo na hisa katika kampuni mbalimbali sasa yatatozwa kodi,
baada ya kufutwa kwa msamaha kwa waliokuwa wakimiliki hisa chini ya asilimia
25.
Katika
kodi inayokatwa katika mishahara (P.A.Y.E), imepunguzwa kutoka asilimia 11
mpaka tisa kwa wafanyakazi wanaopata mshahara wa kuanzia Sh 170,000 lakini
hauzidi 360,000. Kwa wanaopata zaidi ya 360,000 lakini haizidi 540,000,
watakatwa Sh 17,100 pamoja na asilimia 20 ya kiasi kinachozidi Sh 360,000.
Kabla
ya hapo walikuwa wakikatwa Sh 20,900 na asilimia 20 ya kiasi kinachozidi Sh
360,000.
Wanaopata
zaidi ya Sh 540,000 lakini haizidi Sh 720,000, watakatwa Sh 53,100 pamoja na
asilimia 25 ya kiasi kinachozidi 540,000.
Kabla
ya hapo, walikuwa wakikatwa Sh 56,900 na hiyo asilimia 25 ya kiasi kilichozidi
540,000. Kwa wanaopata zaidi ya Sh 720,000 wao watakatwa Sh 98,100 pamoja na
asilimia 30 ya kiasi kinachozidi Sh 720,000.
Kabla
ya hapo, walikuwa wakikatwa Sh 101,900 pamoja na asilimia 30 ya kiasi
kilichozidi Sh 720,000.
Serikali
pia imependekeza malipo ya kupanga nyumba, nayo yatozwe kodi ambayo haikuweka
kiwango, ila imependekeza Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato, apewe mamlaka ya
kukadiria kiwango cha chini na cha juu cha mapato yapatikanayo na pango ili
yatozwe kodi.
Mbali
na mapato ya kodi za nyumba, Serikali imependekeza kupandisha ushuru wa
kusajili magari na pikipiki kutoka Sh 150,000 hadi Sh 250,000 kwa kila gari na
kutoka Sh 45,000 hadi Sh 95,000 kwa kila pikipiki.
Kwa
watumiaji wa namba binafsi za magari, ada sasa itapanda kutoka Sh milioni 5
kila baada ya miaka mitatu mpaka Sh milioni 10.
Aidha,
kodi za majengo sasa hazitakusanywa na halmashauri, badala yake TRA ndiyo
inayopewa mamlaka hayo ya kukadiria, kukusanya, kuhifadhi na kuiwakilisha
katika halmashauri husika.
Mbali
na TRA kupewa mamlaka ya kukusanya kodi ya majengo, serikali pia imependekeza
kupunguza misamaha ya kodi za majengo ili majengo mengi zaidi yaingizwe katika
orodha ya kulipa kodi.
Saruji
aina ya (HS Code 2523.29.00) zinazotoka nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
ushuru wake wa forodha umepandishwa kutoka asilimia 25 mpaka asilimia 35 ili
kulinda saruji inayozalishwa nchini dhidi ya ushindani wa bei ya saruji kutoka
nje ya nchi.
Kwa
bidhaa za chuma ikiwemo mabati kutoka nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, nazo
ushuru umetoka asilimia 0 mpaka 10, ili kulinda uzalishaji wa bidhaa hizo hapa
nchini, huku bidhaa za nondo kutoka nje nazo zikipandishwa kodi kutoka asilimia
10 mpaka 25, kwa nia ya kulinda viwanda vya ndani.
Nyavu
za kuvua samaki kutoka nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, ushuru wake umepanda
kutoka asilimia 10 hadi asilimia 25 huku vichujia vya vilainishi na petroli
kutoka nje ya nchi vikiongezwa ushuru kufikia asilimia 25 kutoka asilimia 10,
ili kulinda bidhaa za ndani.
Katika
sukari, serikali imekusudia kupunguza msamaha wa kodi na hivyo waagizaji wa
bidhaa za sukari kutoka nje watalazimika kuanza kulipa ushuru wa asilimia 15
kutoka asilimia 10, huku ikitarajiwa kuongezeka zaidi na kuwa asilimia 20 mwaka
2017/18 na asilimia 25 mwaka 2018.19, ili kulinda viwanda vya ndani.
Kwa
upande wa ngano kutoka nje, ushuru umepunguzwa kutoka asilimia 35 mpaka 10, kwa
kuwa nchi za Afrika Mashariki hazina uwezo wa kuzalisha kulingana na
mahitaji.
Kwa
upande wa nguo na viatu vya mitumba Serikali imepandisha ushuru kutoka dola za
Marekani 0.2 mpaka dola za Marekani 0.4 kwa kilo, kwa nia ya kudhibiti nguo
hizo lakini pia imetangaza kujiandaa kuzuia uingizaji wake.
Kwa
upande wa mafuta ya kula kutoka nje nayo ushuru umepanda kutoka asilimia 0
mpaka 10 kwa mafuta ghafi ya kula, ili kuimarisha kilimo cha mbegu za mafuta na
viwanda vya ndani.
Miongoni
mwa tozo zilizofutwa kuondoa kero kwa wananchi ni mchango kwa kila kiwanda cha
kuchambua pamba wa Sh 450,000 na ada ya vikao vya halmashauri wakati wa
kujadili wafanyabiashara wa pamba ya Sh 250,000.
Kwa
upande wa kahawa, Serikali imefuta ada ya leseni ya kusindika kahawa ya dola za
Marekani 250, huku ushuru wa kusafirisha korosho wa Sh 50 kwa kilo,
ukifutwa.
Tozo
zingine zilizofutwa katika korosho ni ushuru wa chama kikuu cha ushirika Sh 20
kwa kilo, gharama za mtunza ghala Sh 10 kwa kilo, kikosi kazi cha kufuatilia
masuala mbalimbali Sh 10 na makato ya unyaufu.
Pia
Serikali imepanga kuendelea kufuta tozo nyingine zinazokatwa na halmashauri,
wakala na mashirika katika mazao ya wakulima, baada ya kufanya tathmini za
kina.
Serikali
imependekeza kufuta msamaha wa kodi uliokuwa ukitolewa katika maduka na
migahawa maalumu kwa ajili ya askari wa majeshi, kutokana na msamaha huo
kutumiwa vibaya na kupoteza mapato ya serikali na badala yake, askari watapata
posho mpya juu ya posho ambazo wamekuwa wakipewa.
No comments:
Post a Comment