Meneja wa Afya na Usalama Mahali pa Kazi Kutoka
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Majige Mabula akiongea na
waandishi wa habari (hawapo pichani) ambapo aliwataka wateja wa shirika hilo
kuzingatia sheria na kanuni za matumizi ya umeme ili kuepuka ajali zinazoweza
kusababishwa na hitilafu za umeme.Kulia ni Afisa Uhusiano wa Shirika hilo Bw.
Yasini Silayo.
Shirika la Umeme Tanzania limewataka wateja wake kuzingatia sheria na kanuni za matumizi ya umeme ili kuepuka ajali zinazoweza kusababishwa na hitilafu za umeme.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es salaam na
Meneja wa Afya na Usalama kazini Mhandisi Majige Mabulla wakati wa mkutano na vyombo vya
habari.
Majige amesema kuwa moto hauwezi kutokea endapo mtumiaji wa umeme atahakikisha
kuwa mfumo wa umeme katika nyumba yake umesukwa na fundi ama mkandarasi
aliyesajiliwa.
“Kuwa makini katika matumizi bora ya vifaa
vinavyotumia umeme kama vile pasi,hita za umeme,kuchaji simu,kompyuta
kutasaidia kupunguza au kuondoa tatizo la majanga ya moto” alisisitiza Mabulla.
Akizungumzia hatua nyingine zinazoweza kusaidia
kuzuia majanga ya moto Mhandisi Majige
ni kuepuka kuweka vitu vinavyoweza kushika moto kirahisi karibu na nyaya ama
maungio ya nyaya za umeme ndani ya nyumba .
Majige alitoa wito kwa watumiaji wa umeme kutoa
taarifa pale wanapotaka kuongeza matumizi ya umeme kwa kiwango kikubwa ndani ya
makazi ya watu ili tathmini ya uwezo wa nyaya kukidhi mahitaji yaliyoongezeka
ifanyike.
Katika kuzuia matukio ya moto TANESCO imekuwa
ikihakisha kuwa inamfikishia mteja umeme ulio salama na usiokuwa na madhara kwa
mtumiaji kutoka kwenye nguzo mpaka kwenye mita.
Kwa kipindi kirefu sasa kumekuwepo na matukio ya
ajali za moto katika makazi ya watu ambayo yamekuwa yakisababisha madahara ikiwemo kusababisha vifo,majeruhi na uharibifu wa mali.
No comments:
Post a Comment