KIPA wa Prisons ya Mbeya, leo Benno Kakolanya amesaini Mkataba wa miaka miwili kujiunga na wafalme wa soka ya
Tanzania, Yanga SC.
Usajili huo ni pigo kwa Simba SC ambao pia walikuwa wanamtaka kipa huyo, lakini ‘Chelewa Chelewa, mwana si wao tena” – kwani wenye kisu kikali wamefanya yao.
Akizungumza leo, Kakolanya
amesema kwamba amesaini Yanga baada ya kumaliza Mkataba wake wa miaka mitatu
Prisons ya Mbeya.
“Nimesaini miaka miwili
kujiunga na Yanga, baada ya kumaliza Mkataba wangu Prsons,”amesema kakolanya
ambaye ni kipa wa tatu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.
Kakolanya sasa anakwenda kuungana na makipa watatu waliopo Yanga, Deo Munishi ‘Dida’, Ally Mustafa ‘Barthez’ na Benedicto Tinocco kufanya idadi ya makipa wanne.
Kakolanya sasa anakwenda kuungana na makipa watatu waliopo Yanga, Deo Munishi ‘Dida’, Ally Mustafa ‘Barthez’ na Benedicto Tinocco kufanya idadi ya makipa wanne.
Hata hivyo, mustakabali wa
Tinocco haueleweki sasa baada ya kusajiliwa kwa Kakolanya mwenye umri wa miaka
22, ambaye Prisons ilimuibua Mbaspo Academy.
No comments:
Post a Comment