Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Elias Kyunga.
Wizara ya Afya,maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Shirika lisilo la
kiserikali la ABT ASSOCIATES inategemea
kuendesha zoezi la upuliziaji wa Dawa ya Ukoko majumbani katika halmashauri ya
mji wa Geita, na zoezi hilo linategemea kuanza tarehe 15 juni mwaka huu
Akizindua zoezi hilo
katika viwanja vya halmshauri ya Mji mkoani hapa, mkuu wa mkoa wa Geita, Meja
Jenerali mstafu Ezekiel Elias kyunga, amesema kuwa malaria bado ni ugonjwa
unaoongoza kwa vifo na kwa Tanzania ni
miongoni mwa nchi 10 za Afrika ambapo sehemu kubwa watu wake wapo katika hatari
ya maambukizi ya Malaria, huku zaidi ya asilimia 93 ya wananchi wanaoishi wapo kwenye maeneo yenye hatari ya maambukizi
ya Malaria Nchini.
Kwa upande wake
mwakilishi wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), Bw.Isack Senya,amesema kuwa
lengo la Mgodi kudhamini mradi huo ni kuhakikisha kuwa Wananchi wanaouzunguka Mgodi
wanakuwa katika hali ya usalama na zaidi wanakuwa katika afya njema,na
amewataka wananchi kulipokea zoezi hilo na kukubali kushirikiana na Halmashauri kuhakikisha kuwa wanakuwa
mstari wa mbele kutokomeza malaria katika kaya zao.
Aidha kwa upande wao
wananchi wamesema kuwa wamelipokea zoezi hilo kwa mikono miwili lakini
wameiomba Serikali kuhakikisha kuwa inatoa Elimu ya kutosha kwa wananchi ambao
wapo pembezoni mwa Mji ili kuweza kujinusuru na Janga la Maralia katika maeneo
yaliyopo nje.
Takwimu za Dunia
zinaonyesha kwamba wastani wa mtu mmoja anapoteza maisha kwa kila dakika moja
inayopita kutokana na ugonjwa huu, pia ripoti ya dunia ya shirika la afya
duniani ya mwaka 2012 ambapo malaria iliua takribani watoto laki 4 na elfu
82,000 wenye umri chini ya miaka mitano, Kitaifa inakadiriwa kuwa wastani wa
wagonjwa wapatao elfu 60 hadi 80
hupoteza maisha kutokana na Ugonjwa wa Malaria kwa mwaka.
No comments:
Post a Comment