Kupanda kwa bei ya mazao ya vyakula ikiwemo karanga, viazi, na mihogo, katika kipindi cha
mwezi mtukufu wa ramadhani imeonekana
kuwa ni changamoto kubwa kwa wananchi mkoani geita hususani wenye vipato vya
chini.
Baadhi ya wananchi waishio mkoani Geita
walipokuwa wakizungumza na Storm habari kwa nyakati tofauti wamesema kumekuwepo
na desturi ya baadhi ya wafanyabiashara kupandisha bei
ya vyakula hivyo wakati
wa mfungo wa ramadhani.
Hata
hivyo wananchi hao wameiomba serikali kuhakikisha kuwa inaingilia
kati jambo hilo ikiwa ni pamoja na kudhibiti
ongezeko la bei katika kipindi hiki.
Afisa
biashara wa halmashauri ya mji bw, George Mpogomi amesema kuwa wananchi
walio na bidhaa zinazohitajika kwa kipindi
hiki ni vyema wakaanza kuzipeleka katika masoko
ili kuondoa upungufu wa bidhaa sokoni jambo ambalo husababisha kupanda
kwa gharama za mazao hayo.
Aidha Mpogomi
amewashauri wakulima kutumia fursa hiyo kuuza baadhi ya mazao
ambayo yatawasaidia kunyanyua vipato
vyao.
No comments:
Post a Comment