Friday 10 March 2017

WANANCHI WA MGANZA WAIOMBA SERIKALI KUBORESHA KITUO CHA MABASI YA ABIRIA



Wananchi wa kata ya Mganza  wilayani Chato mkoani Geita  wameiomba Serikali kufanya maboresho  ya kituo cha magari  ya abiria  kutokana na kutokuwepo na kituo rasmi cha kuegesha  magari  hali inayowalazimu madereva wa vyombo hivyo kuegesha magari  pembezoni mwa barabara  pamoja  na kandokando ya makaazi ya watu.
Hali hiyo imekuja   mara baada ya storm fm kuzuru kata ya Mganza  na kujionea madereva wakiegesha magari kandokando ya makazi ya watu huku wengine wakiegesha pembezoni mwa barabara kwa lengo la kusubiria watu wanao safiri.

wakizungumza baadhi ya  wakazi wa maeneo hayo ambapo magari hayo huegeshwa  bi, mwima masatu ,  emanuel mpuya na wengine wengi  wameonekana kukerwa na hali hiyo ambapo wamedai kuwa  ajali za marakwamara zimekuwa zikijitokeza hususani kwa watoto wadogo kutokana na hilo wanaiomba  serikali kuhakikisha inatatua changamoto hiyo.

Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo Bw.  Emanuel mwita amekiri kuwepo kwa hali hiyo na kusema kuwa tayari suala hilo amelifikisha halimashauri ya wilaya ya Chato na kufikia makubaliano ya kuanza ujenzi huo  mara moja.


Aidha Bwana Mwita amewaomba wananchi wake kuwa wavumilivu wakati serikali ikiendelea na utaratibu wa kuanza ujenzi wa kituo kipya cha kuegesha magari katika kata hiyo.

1 comment:

  1. Lakini hapo sio geita ni stend ya tukuyu rungwe mkoani mbeya

    ReplyDelete