KIUNGO mshambuliaji wa
kimataifa wa Zambia, Obrey Chirwaanatarajiwa kuwasili leo Dar es Salaam
kukamilisha usajili wake kujiunga na Yanga SC.
Chirwa alikuwa mshambuliaji pacha wa Donald Ngoma katika klabu ya
FC Platinums ya Zimbabwe.
Na baada ya Ngoma kuhamia Yanga, akawashauri viongozi wa timu hiyo wamchukue winga huyo wa kulia wa timu ya vijana ya Zambia chini ya umri wa miaka 23.
Na baada ya Ngoma kuhamia Yanga, akawashauri viongozi wa timu hiyo wamchukue winga huyo wa kulia wa timu ya vijana ya Zambia chini ya umri wa miaka 23.
Na inaaminika Yanga imekubali kutoa zaidi ya dola za Kimarekani
100 000 kuipata saini ya Chirwa ambaye anatokea FC Platinum ya
Zimbabwe, klabu waliyotokea wachezaji wake wengine, Wazimbabwe Thabani
Kamsuoko na Ngoma.
Mwaka jana, Chirwa alikataa kujiunga na Hobro IK ya Denmark kwa
kutoridhishwa na malipo - na maana yake Yanga itakuwa imempa mshahara
mzuri.
Yanga inataraka kutuma jina la mchezaji huyo Shirikisho la Soka
Afrika (CAF) ili awahi kucheza mechi za Kundi A Kombe la Shirikisho.
Na mpango huo utafanywa mapema tu atakapokamilisha usajili wake
leo
No comments:
Post a Comment