Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt.
John Pombe Magufuli leo Jumamosi tarehe 07 Mei, 2016 amewatunuku Kamisheni
Maafisa wapya 586 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kundi la 58/15
waliomaliza mafunzo yao katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli (TMA) Mkoani
Arusha.
Maafisa hao wapya wa Jeshi walianza kozi yao tarehe 04 Mei, 2015 na wamepewa
cheo cha Luteni usu.
Kati ya maafisa wapya waliohitimu kozi yao leo, 80 ni madaktari
na 6 ni marubani wa ndege waliopata mafunzo yao katika nchi tatu ambazo ni
Tanzania, Uganda na Afrika Kusini.
Kabla ya kutunuku Kamisheni kwa maafisa hao, Rais Dkt. John
Pombe Magufuli amekagua gwaride la maafisa hao wapya na pia amepokea heshima ya
gwaride lililopita mbele yake kwa mwendo wa pole na haraka, na baadaye
kusikiliza ujumbe juu ya utendaji kazi wa serikali ya awamu ya tano, nidhamu ya
kazi na uzalendo kupitia muziki wa bendi na kwaya.
Katika hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli kwa mara nyingine amelazimika kuzungumza na wananchi
wa Arusha Mjini waliokuwa wamezuia msafara wake uliokuwa ukitoka Chuo cha
Mafunzo ya Kijeshi Monduli kwenda Ikulu ndogo ya Arusha, na kuwahakikishia kuwa
serikali yake imeanza kuwashughulikia wafanyabiashara ambao wameficha sukari
kwa makusudi na kusababisha upungufu wa bidhaa hiyo.
Rais Magufuli amesema tayari vyombo vya dola vimekamata tani
5,000 za sukari iliyofichwa na mfanyabiashara mmoja huko Tabata Jijini Dar es
salaam na pia vimembaini mfanyabiashara mwingine aliyeficha sukari hiyo Jijini
Arusha.
"Kweli
nitawakomesha hawa, wasije wakanilaumu, haiwezekani ukaficha sukari wakati
viwanda vyetu vinatengeneza sukari, kuna mmoja mwingine yupo Arusha hapa, nae
ameficha sukari, alienda akanunua kwenye viwanda vya sukari vya hapa akaificha
yote, leo ninamshughulikia.
"Kuna mwingine
alinunua sukari pale Kilombero zaidi ya tani 3,000 akaficha, na mwingine ameshikwa
pale Tabata alikuwa ameficha tani 5,000, na wanasubiri katika mwezi Mtukufu wa
Ramadhani ili ndugu zetu Waislamu wapate shida, haya ni mashetani makubwa,
unawafichia watu chakula ambacho wanatakiwa kula, lakini nataka niwahakikishie
ndugu zangu, hili ni tatizo la muda Tanzania, sukari itapatikana kwa wingi, na
itanunuliwa na serikali, tumeshaagiza sukari lakini hatutawapa vibali hawa
wafanyabiashara ambao wanatunyonya, tutanunua wenyewe na tutauza bei ya chini, hilo ndio lengo la serikali" Amesema Rais Magufuli
Aidha, Rais Magufuli amerejea kauli yake kuwa serikali yake
haitawavumilia viongozi na watumishi wa umma ambao wamekuwa wakijihusisha na
vitendo vya rushwa na ufisadi, huku akisema ataendelea kutumbua majipu kwa
yeyote atakayebainika kuchezea mali za umma ili kulinda maslai ya wengi,
hususani watanzania wanyonge.
"Ninafanya kwa niaba yenu, ninafanya kwa niaba yenu, ningekuwa sifanyi
kwa niaba yenu, na mimi ningeingia madarakani ningeanza kushirikiana na hao, na
wengine walifikiria nitashirikiana nao, wamekwama mimi nitawatumbua kila siku
ili Tanzania iwe ya neema iweze kwenda mbele, haiwezekani nchi kama hii tajiri,
Tanzanite ipo, dhahabu ipo, wanyama mpaka nyani wameanza kuuzwa, wakimalizika
nyani
No comments:
Post a Comment