Serikali imesema kuwa mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM)umekubali kutoa miamba taka(magwangala) kwa ajili ya wananchi mkoani hapa hivyo
ni vyema kwa serikali ya mkoa kuhakikisha kuwa inatafuta eneo kwa
ajili ya shughuli ya uchenjuaji.
Hayo yamesemwa na Waziri wa nishati na madini Prof.Sospeter
Muhongo wakati wa kikao na wachimbaji kilichofanyika
katika ukumbi wa mkoa wa Geita,amesema kuwa swala la magwangala mwisho wake na majibu yake yatapatikana tarehe 30 ya
mwezi wa sita endapo eneo ambalo
litapatikana litakuwa limekidhi vigezo na sheria na kuwepo kwa usalama kwa eneo hilo.
Aidha Waziri
Muhongo ameutaka mgodi wa dhahabu (GGM)katika kikao cha tarehe 30 kuhakikisha kuwa wanaonesha ni
kiasi gani cha fedha walizotoa katika maendeleo ya mkoa kwa kipindi cha miaka
mitano.
Kwa upande wao wabunge wa majimbo yote ya Geita
waliokuwepo katika kikao hicho wametoa maoni yao tofauti juu ya kauli ya kutolewa
kwa miamba taka tarehe 30 june.
No comments:
Post a Comment