Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli ametangaza kushusha kodi ya
mapato ya Mshahara ( Pay as you Earn -PAYE ) kutoka asilimia 11
iliyopo sasa hadi asilimia 9.
Rais amesema ameamua
kuchukua umamuzi huo ili kutimiza ahadi yake aliyoitoa wakati wa kampeni ya
kuwapunguzia mizigo wafanyakazi kwa kuwaongezea mishahara na kuwapunguzia kodi
ya mapato ya mishahara.Kuhusu kuwaongezea mishahara, Rais Magufuli ameomba wafanyakazi wamvumilie kwa kuwa hivi sasa yuko kuimarisha uchumi wa nchi kwa kuziba mianya yote ya Rushwa.
Katika hatua nyingine,
Rais Magufuli amewataka waajiri wote nchini kuwapa wafanyakazi wao mikataba ya
ajira na kupeleka makato yao kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii bila kukosa
No comments:
Post a Comment