Kikosi cha timu ya soka ya Serengeti Boys.
Serengeti Boys imecheza mfululizo
michezo 7 ya kimataifa bila kufungwa dhidi ya Misri (2), India, Kore, Malaysia,
na Marekani (USA).
Kabla ya hapo timu hiyo ilicheza
michezo kadhaa ya ndani na timu za chini ya umri wa miaka 20 bila kupoteza hata
mchezo mmoja.
Mratibu wa timu ta Tanzania kutoka
Shirikisho la Soka la Kenya, Anthony Achia, amesema walikuwa wanafuatilia
michuano hiyo na mafanikio ya Serengeti.
“Timu imefanya vema, ikitunza hii
inaweza kuitoa Afrika Mashariki kimasomaso. Unajua sisi sote ni wa East Africa
(wa Afrika Mashariki). Sasa ukiona mwezako anafanya vema, lazima useme.
Endeleeni. Itakuja kuirithi hii”
Katika mashindano ya AIFF, timu hiyo
pekee kutoka Afrika na ambayo ilikua kipenzi cha mashabiki katika jiji la Goha
ilicheza na timu ambazo ziko juu katika hatua za juu katika mtoano wa kuwania
kushiriki Kombe la Dunia kupitia mabara yao yaani CONCACAF (USA) na AFC (India,
Korea na Malaysia).
Haishangazi nchi nyingi za Ulaya,
Asia na Marekani zimeulizia uwezekano wa timu hii kutembelea nchi zao kwa
michezo ya kirafiki.
Awali timu ya Serengeti Boys ilipewa
nafasi ndogo ya kufanya vizuri kwa sababu ya rekodi zilizokuwa zinaiweka
Tanzania katika viwango vya chini katika umri huo kwa nchi za Afrika Magharibi
na Kaskazini zilikuwa juu zaidi na vilevile ukweli wa kwamba timu kama USA,
Korea, Malasyia na India zilikuwa na bajeti kubwa iliyogharamiwa na Serikali
zao na walikuwa na vifaa vya kila namna kiasi cha kuomba magari kwa ajili ya
vifaa vya mazoezi na mechi.
Kikosi cha Serengeti kinavunja kambi
kabla ya kurejea siku si nyingi ili kujiandaa na mchezo wa kufuzu fainali za
Afrika chini ya miaka 17 (Madagascar 2017) dhidi ya Ushelisheli hapa tarehe 25
Juni katika uwanja wa Taifa Dar es salaam.
Benchi la ufundi limeahidi kuendelea
kukiimarisha kikosi hiki na vilevile kutengeneza mpango endelevu wa kuwa na
wachezaji bora zaidi kila mwaka.
Serengeti Boys ilimaliza Mashindano
ya AIFF katika nafasi ya tatu kwa kuifunga Malaysia mabao 3-0.
Serengeti Boys na Bingwa Korea
hawakupoteza mchezo hata mmoja na awali walipokutana walitoka sare ya 2-2.
No comments:
Post a Comment