Wito huo umetolewa na
mwenyekiti wa Kamati ya sherehe hizo ambae ni mkuu wa wilaya hiyo,mh amani
mwenegoha wakati wa zoezi la kufanya tathimini na mapendekezo ya miradi itakayozinduliwa
na kuwekewa jiwe la msingi wakati wa mbio hizo.
Awali mratibu wa mbio
za Mwenge wilayani hapo, Elimkwasa John wakati akiwasilisha miradi iliyopendekezwa
mbele ya viongozi na Wakuu wa idara mbalimbali .
Ameitaja miradi iliyopendekezwa ili ijadiliwe na kufanyiwa maboresho na mapendekezo
kuwa ni soko la wakulima wa mihogo kijijini Namonge,mradi wa ujenzi wa nyumba
za walimu katika shule ya sekondari Namonge , ujenzi wa Barabara ya Uyovu Kabagore
na Kayenze pamoja na ukarabati wa chumba cha upasuaji katika kituo cha afya cha
Uyovu.
Aidha John amesema kuwa
Mwenge unatarajia kuingia Wilayani Bukombe ukitokea Biharamlo mkoani Kagera
ukibeba kauli mbiu isemayo vijana ni nguvu kazi ya taifa washirikishwe na
kuwezeshwa .
No comments:
Post a Comment