Akisoma maamuzi hayo ya Bunge Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge
ya Haki, Kinga, Maadili na Madaraka ya Bunge, George Mkuchika amesema Januari
27.01.2016 wabunge hao walikiuka sheria na taratibu za kuongoza bunge kwa
walishinikiza kiti cha spika kijadili hoja ambayo ilikwisha tolewa uamuzi na
kiti hicho.
Wabunge waliosimamishwa kuhudhuria vikao hivyo ni Zitto
Kabwe, John Heche, Halima Mdee, Tundu Lissu, Godbless Lema, Pauline Gekul na
Esther Bulaya.
Azimio la adhabu kwa wabunge hao limetolewa na Bunge chini
ya Kifungu cha 30A (1) cha sheria ya Haki Kinga na Madaraka ya Bunge Sura ya
296 na kanuni ya 74 (4) na (6).
Kufuatia uchunguzi huo Bunge kupitia kamati hiyo limeazimia
kuwa Ester Bulaya naTundu Lisu wasihudhurie vikao vyote vya mkutano wa tatu wa
Bunge la Kumi na Moja vilivyobaki kuanzia tarehe 30 Mei , 2016 pamoja na vikao
vyote vya Mkutano wa Nne Spika wa Bunge la Kumi na Moja kwa kuwa walipatikana
na makosa ya ukiukwaji wa Kanuni na kuonyesha dharau kubwa kwa mamlaka ya
Bunge.
Aidha, Bunge limeazimia kuwa Mhe. Pauline Gekul,
Mhe.Godbless Lema, Mhe.Zitto Kabwe na Mhe Halima Mdee wasihudhurie vikao vyote
vya mkutano wa tatu wa Bunge kuanzia tarehe 30 Mei 2016.
Adhabu hizo Bunge limeazimia Mhe.John Heche asihudhurie
vikao kumi mfululizo vya Mkutano wa Tatu wa Bunge hilo kuanzia Mei, 30, 2016
kwa kuwa alipatikana na kosa moja.
No comments:
Post a Comment