Mchezo huo utapigwa kesho kuanzia saa 10:30 jioni kwenye
Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam huku waamuzi wasaidizi watakuwa Ferdinand
Chancha wa Mwanza (line 1) na upande wa pili ni Soud Lila wa Dar es Salaam
(line 2) na mwamuzi wa akiba ni Frank Komba wa Dar es Salaam pia na Kamishna wa
mchezo huo atakuwa Juma Mgunda wa Tanga.
huyo ambaye sasa wanakutana naye tena akichezesha mchezo
huo dhidi ya timu ile ile ya Azam.
Kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu
msimu wa 2015/16, mabingwa wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara msimu wa 2015/16
wataiwakilisha nchi katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2016/17
ambapo nafasi hiyo tayari imechukuliwa na Young Africans.
Kadhalika Azam ina tiketi tayari ya
kushiriki Kombe la Shirikisho Barani Afrika kwa kufika fainali za ASFC ingawa
kanuni zinataka bingwa ambako kwa upande wa Yanga wana tiketi ya michuano ya
juu zaidi ya shirikisho. Mvuto wa mchezo wa Jumatano ni ushindani wa soka na
zawadi kwa bingwa.
Fainali za Kombe la Shirikisho
zinakuja baada ya mchuano ulioshindanisha timu 64 za Ligi Kuu Tanzania Bara -
VPL (16); Ligi Daraja la Kwanza -FDL (24), Ligi Daraja la Pili – SDL (24).
No comments:
Post a Comment