Wananchi wa mtaa wa
Mwatulole mkoani Geita wamemtaka
Afisa ardhi wa Halmashauri ya mji wa Geita Bw.Mabula Gogodi kuwapatia
maelezo ya kina kuhusu kupima ramani za Barabara za mtaa huo bila
kuwashirikisha hali ambayo imepelekea huduma za kijamii kusuasua.
Afisa huyo, amejikuta
akiwa katika wakati mgumu mbele ya mwenyekiti
mtaa huo, Charles Fikiri, ambapo sauti yao ilikuwa ni moja tu ni kwanini
apime viwanja na kuzigeuza baadhi ya barabara kuwa viwanja vya kujenga makazi
ya watu.
Afisa huyo amegoma
kuzungumza na storm habari kwa kigezo
kuwa yeye si msemji, lakini kinasa sauti iliweza kunasa mazungumzo yake wakati akiwafafanulia
wananchi baadhi ya mambo.
Aidha kwa upande wake
mwenyekiti wa mtaa wa Mwatulole Charles Fikiri,amesema kuwa wakati wa ramani
zinapochorwa mara nyingi mipango miji wamekuwa hawashirikishi jamii na mwisho
wa siku matatizo kama hayo hujitokeza mara kwa
mara.
Hadi storm habari
inaondoka katika eneo la tukio imeshuhudia
wananchi wakiondoa vigingi vya mawe katika eneo ambalo linasadikika
ndipo ilipokuwa barabara na kugeuzwa uwanja
wa makazi.
No comments:
Post a Comment