Meneja Mawasiliano wa
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) Bw. David Mziray
akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa
wadau wa usafiri wakiwamo SUMATRA, UDA, DART na Jeshi la Polisi.
Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) Bw. Giliard Ngewe
akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu nauli zitakazotumika
katika mradi wa mabasi yaendayo haraka unaotarajiwa kuanza rasmi Mei 10, 2016.
Kushoto ni Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi kutoka SUMATRA Bw. Nahson Sigala.
Mkurugenzi wa Udhibiti
Uchumi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) Bw.
Nahson Sigala akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu viwango vipya vya nauli
baada ya SUMATRA kufanya tathmini ya viwango vya nauli iliyopendekezwa awali na
Kampuni ya Usafirishaji ya UDA-RT na kubaini kuwa gharama zilizopendekezwa ni
kubwa mno. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na
Nchi Kavu (SUMATRA) Bw. Giliard Ngewe.
Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) Bw. Giliard Ngewe
(Kulia) na Kaimu Mtendaji Mkuu DART Bw. Ronald Lwakatare wakimkabidhi leseni ya
usafirishaji Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Usafirishaji
No comments:
Post a Comment