Wananchi wa mtaa
wa Nyakato kata ya Nyangoko wilayani na
mkoani Geita,wameishukuru halamshauri ya
mji na diwani wa kata hiyo kutokana na jitihada ambazo wamezifanya za kuhakikisha kuwa kisima cha
maji kinapatikana katika mtaa huo.
Wakizungumza na Storm habari,baadhi ya wananchi wa
mtaa huo,wamesema kuwa ni kwa muda mrefu
wamekuwa wakikutana na adha kubwa kutokana na ukosefu wa maji katika mtaa huo lakini
kwa sasa kutokana na kufunguliwa kwa
kisima cha maji kitawasaidia kutumia kwa shughuli za nyumbani.
Mwenyekiti wa mtaa huo,Charles Kulola amesema kuwa mradi huo utawanufaisha
wananchi zaidi ya elfu 2,600,na mwalimu wa shule ya msingi Nyakato Peter Mpandoji yeye ameelezea namna ambavyo wanafunzi walikuwa wakikumbana
na adha kutokana na kuwepo kwa uhaba wa
maji hali ambayo ilikuwa ikisababisha wanafunzi
wengi kuwa watoro.
Aidha kwa upande
wake diwani wa kata ya Nyangoko,Elias
Ngole amesema kuwa mradi huo ni moja kati ya mwendelezo wa halmashauri wa kuhakikisha kuwa wanatumia
mapato ya ndani na kiasi cha sh,milioni thelathini zimetumika kutengeneza mradi huo.
No comments:
Post a Comment