Wafanyabiashara wa sukari mkoani Geita wameiomba
serikali pindi itakapoanza zoezi la kuongeza sukari kutoka katika viwanda vya
nje ya nchi kupunguza gharama za manunuzi ya bidhaa hiyo ili waweze kuuza kwa
shilingi 1800 kwa kilo kama bei elekezi tofauti na ilivyo sasa.
Hayo yamesemwa na wafanyabiashara kwa nyakati
tofauti walipokuwa wakizungumza na storm habari mapema hii leo mkoani hapa.
Akizungumza kwa njia ya simu kaimu afisa biashara wa
halmashauri ya mji wa Geita bw, George Mpogomi, amesema kuwa upangaji wa bei ya
sukari unategemea gharama za ununuaji wa bidhaa yenyewe kutoka katika sehemu
husika.
Awali waziri mkuu wa Tanzania mh, Kassim Majaliwa
akiwa katika bunge la 11 alitangaza kuagiza sukari kiasi kutoka katika viwanda
vya nje ili kupunguza adha ya kupanda kwa bei ya sukari nchini huku akiwataka wafanyabiashara
kuacha kupandisha bei ya sukari kiholela bila ya kufuata utaratibu.
No comments:
Post a Comment