Mamlaka ya
mapato Tanzania (TRA) imebakiza Tsh. Trilioni 2.363 ili kufikia lengo
waliojiwekea la kukusanya mapato ya trilioni 12.363 katika mwaka wa fedha
2015/16, ambapo hadi sasa imekusanya kiasi cha Tsh. Trilioni 10.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa awamu ya pili ya mpango wa
mafunzo kwa wafanyakazi waliopo kwenye fursa ya ajira za taasisi hiyo
Kamishina Mkuu wa TRA Bw. Alphayo Kidata alisema taasisi yake imefanikiwa
kukusanya kiasi cha sh trilioni 10 katika muda waliojiwekea na kuahidi
kumalizia kiasi cha shilingi trilioni 2.363 kabla ya mwaka mpya wa fedha wa
Serikali unaoanza mwezi Julai mwaka huu.
“Tumejiwekea malengo ya kukusanya kiasi cha
fedha cha shilingi trilioni 12.363 kwa mwaka huu wa fedha na tumefanikiwa
kukusanya shilingi trilioni 10 mpaka mda huu ila tunaendelea na kutimiza lengo
letu hadi kufikia July mwaka huu na tutajipanga upya mwaka ujao wa fedha
kufikia malengo mapema” alisema
Bw. Kidata.
Aidha Bw. Kidata
amesema kuwa kwa mpango huo wa mafunzo ulioanzishwa kwa kushirikiana na
Chuo cha Usimamizi wa Kodi (ITA) ni mafunzo ya mwaka mmoja yanayoendana na
usaili mpya kwa wahitimu ili kufanya Mamlaka hiyo kuwa na wafanyakazi
waadilifu na wachapa kazi ili kupaisha uchumi nchi.
Kwa upande wake Mkuu
wa chuo cha cha Usimamizi wa Kodi (ITA) Prof. Isaya Jairo alisema kuwa wameamua
kuanzisha mpango huo kwa kushirikiana na Mamlaka ya mapato ili kufundisha
wafanyakazi wa TRA maadili na nyenzo za utendaji kazini pamoja na
kuendesha mafunzo ya dini ili kuwafanya wafanyakazi wawe wacha mungu katika
kazi zao.
Aidha Kaimu Mkurugenzi
Rasilimali Watu na Utawala wa TRA Bw. Victor Kimaro aliwataka wafanyakazi wote
wanatakiwa wafanye kazi kwa maadili hususani upande wa ukusanyaji kodi na Chuo
hicho kimewafundisha wafanyakazi hao kufanya kazi kwa ushindani katika maeneo
ya kazi ili kuliletea taifa maendeleo yaliyokusudiwa.
Kamishina Mkuu wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata (katikati) akionesha kitabu
cha mtaala mpya wa mafunzo kwa wafanyakazi (TRA) watakaopata fursa za kusoma
katika Chuo cha Usimamizi wa Kodi (ITA), kulia ni Mkuu wa Chuo hicho Prof.
Isaya Jairo na kushoto na kushoto ni Kaimu Mkurugugenzi Rasilimali Watu na
Utawala Bw. Victor Kimaro.
Baadhi ya
washiriki waliohudhuria katika uzinduzi wa awamu ya pili ya mpango wa
mafunzo ya kuhitimu kwa wafanyakazi waliopo kwenye fursa za ajira Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) uliofanyikia jijini Dar es salaam.
Baadhi ya washiriki
wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni Rasmi Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata
No comments:
Post a Comment